Januari 26, 2016 ilifika miaka thelathini tangu Rais Yoweri Museveni [1] na chama chake cha National Resistance Movement [2] kuchukua madaraka nchini Uganda, baada ya miaka mitano ya vita viliyomng'oa Rais wa kipindi hicho Milton Obote [3]. Obote aliondolewa madarakani na Idi Amin [4] (1971–79), na alirudi madarakani baada ya Amin mwenyewe kupinduliwa tena toka madarakani.
Mwaka ambao Museveni alikuja kuiongiza nchi, zaidi ya asilimi 75% ya watu wote walioko nchini kwa wakati huu walikuwa hawajazaliwa lakini ndio waliokuwa akitumia hashtag #pichaya1986 [5]kushirikishana kumbukumbu zao za kipindi hicho.
Kwa nini iwe sasa? Rais Museveni anatafuta nafasi [6]ya kurudi madarakani kwa muhula wa sita sasa. Uchaguzi wa Rais [7] utafanyika ifikapo Februari 18, 2016 ambapo waliopo madarakani watadaikushinda [8] katika uchaguzi, hapa inaonekana kuna kutenguliwa kwa kiini macho kikubwa [9] cha shughuli na hatua zote za uchaguzi
Tayari kumeshakuwa na migogoro nchini — kwani afya ya uchumi wa nchi [10]ipo mashakani, kuna taarifa [11] za kwamba Rais Museveni ametumia fedha zaidi ya dola milioni saba( $7) katika kampeni zake za kutafuta kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miezi miwili tu na moja kati ya wapinzani wa Rais wa kisiasa Amama Mbabazi [12], amemtuhumu Museveni [13] kwa kuachilia “kashfa” kwa ajili ya kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wanaowaunga mkono wapinzani.
Watumiaji wa mitandao — ambao wanaoweza kwenda au kutokwenda kupiga kura siku ya uchaguzi wameamua kupaza sauti zao ili zisikike mtandaoni:
Nilikuwa na miaka miwili wakati @KagutaMuseveni [14] alipoingia madarakani. Sasa nina miaka 31. Hashtag #pichaza1986 [5] & shirikisha hadithi yakopic.twitter.com/ipFFiMkWZ0 [15]
— Thomas Ddumba (@tomddumba) January 16, 2016 [16]
#pichaza1986 [17] Huyo ni mimi wakati #M7 [18] alipoahidi kuwa baada ya miaka mitano ataenda kuchunga ng'ombe wake. pic.twitter.com/vhtq1YH41h [19]
— Baksi (@juanbaksi) Januari 19, 2016 [20]
Huyo ni mimi wakati #M7 [18] aliahidi kuwa baada ya miaka mitano ataenda kuchunga ng'ombe wake.
Hivi ndivyo Uganda inakumbuka jinsi Museveni alivyopokelewa madarakani na mataifa ya Magharibi:
#TBT [21] Rais wa zamani wa Marekani akipeana mikono na Rais @KagutaMuseveni [14] pic.twitter.com/OWpZGehsKs [22]
— Hii ndio Uganda (@HiindioUganda_) Januari 21, 2016 [23]
Rais wa zamani wa Marekani akipeana mikono na Rais @KagutaMuseveni [14]
Wengine walikumbuka jinsi familia zao zilivyolazimika kukimbilia nchi za Magharibi:
#pichaza1986 [5]Dada yangu @barnta [24] na mimi, huko Kingston, Ontario, nchini Kanada. Wazazi wangu walikuwa uhamishoni :)))) pic.twitter.com/fNF1LgtQmU [25]
— Kasabiiti (@Kasabiiti) Januari 17, 2016 [26]
Dada yangu @barnta [24] na mimi, huko Kingston, Ontario, nchini Kanada. Wazazi wangu walikuwa uhamishoni
#Pichaza1986 [5] albamu ya familia iliyopotelea uhamishoni
— emmanuel othini (@EOthini) Januari 17, 2016 [27]
#Pichaza1986 albamu ya familia iliyopotelea uhamishoni
Pia kulikuwa na mlinganisho wa “kipindi hicho” na “sasa”:
#pichaza1986 [17] linganisha Museveni wa leo na yule wa 1986pic.twitter.com/XPfAX8royw [28]
— mirugwe alex junior (@mirugwealex1) Januari 19, 2016 [29]
Hebu linganisha Museveni wa leo na yule wa 1986
#pichaza1986 [5] Hii ingetosha kununua gari. Kwa sasa inanunua yai tu! pic.twitter.com/rDDlkHLgA3 [30]
— Kityo Kenny Rand (@kkennyrand) Januari 18, 2016 [31]
Hii ingetosha kununua gari. Kwa sasa inanunua yai tu!
Kalundi Serumaga alikumbukia enzi zake akiwa kwenye Chama cha Ukombozi wa Uganda/( Uganda National Liberation Front):
@dfkm1970 [32] Hakuna picha, ila ilikuwa sehemu ndogo ya UNLF(A-D), nikipigana na NRM, nilishapihana na madikteta wengine kabla ya hiyo. #pichaza1986 [17]
— Kalundi Serumaga (@NativeLandgrab) Januari 17, 2016 [33]
Hakuna picha, ila ilikuwa sehemu ndogo ya UNLF(A-D), nikipigana na NRM, nilishapihana na madikteta wengine kabla ya hiyo
Mtumiaji wa Twitter Charles Onyango-Obbo alibandika picha ya kumomonyoka au uharibifu wa ziwa Victoria na kuifanyia mfananisho wa kisiasa:
Circa mwaka 1986 Ziwa Victoria lenye afya • 2016 magugu maji hayo yamekabwa na maji karibu kufa (kiashiria kizuri!) #pichaza1986 [5] pic.twitter.com/OtFzCsqx5Y [34]
— Charles Onyango-Obbo (@cobbo3) Januari 19, 2016 [35]
Circa mwaka 1986 Ziwa Victoria lenye afya • 2016 magugu maji hayo yamekabwa na maji karibu kufa (kiashiria kizuri!)
Watumiaji wengi wa Twitter wanafikiri kuwa mbio za miaka 30 zinatosha kabisa:
#pichaza1986 [17]. Siku nzuri za zamani… :-) miaka 30 ni kipindi kirefu sana, ni muda mrefu! pic.twitter.com/QXBMYQVf5u [36]
— Ronald Sebuhinja K (@sebsronnie) Januari 17, 2016 [37]
Siku nzuri za zamani… :-) miaka 30 ni kipindi kirefu sana, ni muda mrefu!
Bado sijakutana na Mganda ambaye amekuwa akifanya kazi moja tu kwa miaka 30, lakini asiwe @KagutaMuseveni [14] #1986Pictures [17]
— Thomas Ddumba (@tomddumba) Januari 18, 2016 [38]
Bado sijakutana na Mganda ambaye amekuwa akifanya kazi moja tu kwa miaka 30, lakini asiwe @KagutaMuseveni [14]
#pichaza1986 [17] imepindishwa kidogo pic.twitter.com/t5HzuPvrsV [39]
— Aguma Awoii (@AwoiiKen) Januari 20, 2016 [40]
#Pichaza1986 imepindishwa kidogo
Bandiko moja tu huko tweeter, lakini, limeamsha hisia na kuonesha kiwango cha fadhaa wanayoweza kuwa wanaisikia vijana wengi wa Uganda:
Mwaka 1986 baba yangu na mama hawakuwa wamekutana hivyo sikuwa hata kwenye mpango ila najisikia kuchoka kuliko hao waliokuwepo kabla yangu #pichaza1986 [17] unaugusa moyo wangu 😓😫😭😥
— Shannah Namaganda Am (@shannah2012) Januari 20, 2016 [41]
Mwaka 1986 baba yangu na mama hawakuwa wamekutana hivyo sikuwa hata kwenye mpango ila najisikia kuchoka kuliko hao waliokuwepo kabla yangu #pichaza1986 [17] unaugusa moyo wangu