Januari 26, 2016 ilifika miaka thelathini tangu Rais Yoweri Museveni na chama chake cha National Resistance Movement kuchukua madaraka nchini Uganda, baada ya miaka mitano ya vita viliyomng'oa Rais wa kipindi hicho Milton Obote. Obote aliondolewa madarakani na Idi Amin (1971–79), na alirudi madarakani baada ya Amin mwenyewe kupinduliwa tena toka madarakani.
Mwaka ambao Museveni alikuja kuiongiza nchi, zaidi ya asilimi 75% ya watu wote walioko nchini kwa wakati huu walikuwa hawajazaliwa lakini ndio waliokuwa akitumia hashtag #pichaya1986kushirikishana kumbukumbu zao za kipindi hicho.
Kwa nini iwe sasa? Rais Museveni anatafuta nafasiya kurudi madarakani kwa muhula wa sita sasa. Uchaguzi wa Rais utafanyika ifikapo Februari 18, 2016 ambapo waliopo madarakani watadaikushinda katika uchaguzi, hapa inaonekana kuna kutenguliwa kwa kiini macho kikubwa cha shughuli na hatua zote za uchaguzi
Tayari kumeshakuwa na migogoro nchini — kwani afya ya uchumi wa nchiipo mashakani, kuna taarifa za kwamba Rais Museveni ametumia fedha zaidi ya dola milioni saba( $7) katika kampeni zake za kutafuta kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miezi miwili tu na moja kati ya wapinzani wa Rais wa kisiasa Amama Mbabazi, amemtuhumu Museveni kwa kuachilia “kashfa” kwa ajili ya kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wanaowaunga mkono wapinzani.
Watumiaji wa mitandao — ambao wanaoweza kwenda au kutokwenda kupiga kura siku ya uchaguzi wameamua kupaza sauti zao ili zisikike mtandaoni:
Nilikuwa na miaka miwili wakati @KagutaMuseveni alipoingia madarakani. Sasa nina miaka 31. Hashtag #pichaza1986 & shirikisha hadithi yakopic.twitter.com/ipFFiMkWZ0
— Thomas Ddumba (@tomddumba) January 16, 2016
#pichaza1986 Huyo ni mimi wakati #M7 alipoahidi kuwa baada ya miaka mitano ataenda kuchunga ng'ombe wake. pic.twitter.com/vhtq1YH41h
— Baksi (@juanbaksi) Januari 19, 2016
Huyo ni mimi wakati #M7 aliahidi kuwa baada ya miaka mitano ataenda kuchunga ng'ombe wake.
Hivi ndivyo Uganda inakumbuka jinsi Museveni alivyopokelewa madarakani na mataifa ya Magharibi:
#TBT Rais wa zamani wa Marekani akipeana mikono na Rais @KagutaMuseveni pic.twitter.com/OWpZGehsKs
— Hii ndio Uganda (@HiindioUganda_) Januari 21, 2016
Rais wa zamani wa Marekani akipeana mikono na Rais @KagutaMuseveni
Wengine walikumbuka jinsi familia zao zilivyolazimika kukimbilia nchi za Magharibi:
#pichaza1986Dada yangu @barnta na mimi, huko Kingston, Ontario, nchini Kanada. Wazazi wangu walikuwa uhamishoni :)))) pic.twitter.com/fNF1LgtQmU
— Kasabiiti (@Kasabiiti) Januari 17, 2016
Dada yangu @barnta na mimi, huko Kingston, Ontario, nchini Kanada. Wazazi wangu walikuwa uhamishoni
#Pichaza1986 albamu ya familia iliyopotelea uhamishoni
— emmanuel othini (@EOthini) Januari 17, 2016
#Pichaza1986 albamu ya familia iliyopotelea uhamishoni
Pia kulikuwa na mlinganisho wa “kipindi hicho” na “sasa”:
#pichaza1986 linganisha Museveni wa leo na yule wa 1986pic.twitter.com/XPfAX8royw
— mirugwe alex junior (@mirugwealex1) Januari 19, 2016
Hebu linganisha Museveni wa leo na yule wa 1986
#pichaza1986 Hii ingetosha kununua gari. Kwa sasa inanunua yai tu! pic.twitter.com/rDDlkHLgA3
— Kityo Kenny Rand (@kkennyrand) Januari 18, 2016
Hii ingetosha kununua gari. Kwa sasa inanunua yai tu!
Kalundi Serumaga alikumbukia enzi zake akiwa kwenye Chama cha Ukombozi wa Uganda/( Uganda National Liberation Front):
@dfkm1970 Hakuna picha, ila ilikuwa sehemu ndogo ya UNLF(A-D), nikipigana na NRM, nilishapihana na madikteta wengine kabla ya hiyo. #pichaza1986
— Kalundi Serumaga (@NativeLandgrab) Januari 17, 2016
Hakuna picha, ila ilikuwa sehemu ndogo ya UNLF(A-D), nikipigana na NRM, nilishapihana na madikteta wengine kabla ya hiyo
Mtumiaji wa Twitter Charles Onyango-Obbo alibandika picha ya kumomonyoka au uharibifu wa ziwa Victoria na kuifanyia mfananisho wa kisiasa:
Circa mwaka 1986 Ziwa Victoria lenye afya • 2016 magugu maji hayo yamekabwa na maji karibu kufa (kiashiria kizuri!) #pichaza1986 pic.twitter.com/OtFzCsqx5Y
— Charles Onyango-Obbo (@cobbo3) Januari 19, 2016
Circa mwaka 1986 Ziwa Victoria lenye afya • 2016 magugu maji hayo yamekabwa na maji karibu kufa (kiashiria kizuri!)
Watumiaji wengi wa Twitter wanafikiri kuwa mbio za miaka 30 zinatosha kabisa:
#pichaza1986. Siku nzuri za zamani… :-) miaka 30 ni kipindi kirefu sana, ni muda mrefu! pic.twitter.com/QXBMYQVf5u
— Ronald Sebuhinja K (@sebsronnie) Januari 17, 2016
Siku nzuri za zamani… :-) miaka 30 ni kipindi kirefu sana, ni muda mrefu!
Bado sijakutana na Mganda ambaye amekuwa akifanya kazi moja tu kwa miaka 30, lakini asiwe @KagutaMuseveni #1986Pictures
— Thomas Ddumba (@tomddumba) Januari 18, 2016
Bado sijakutana na Mganda ambaye amekuwa akifanya kazi moja tu kwa miaka 30, lakini asiwe @KagutaMuseveni
#pichaza1986 imepindishwa kidogo pic.twitter.com/t5HzuPvrsV
— Aguma Awoii (@AwoiiKen) Januari 20, 2016
#Pichaza1986 imepindishwa kidogo
Bandiko moja tu huko tweeter, lakini, limeamsha hisia na kuonesha kiwango cha fadhaa wanayoweza kuwa wanaisikia vijana wengi wa Uganda:
Mwaka 1986 baba yangu na mama hawakuwa wamekutana hivyo sikuwa hata kwenye mpango ila najisikia kuchoka kuliko hao waliokuwepo kabla yangu #pichaza1986 unaugusa moyo wangu 😓😫😭😥
— Shannah Namaganda Am (@shannah2012) Januari 20, 2016
Mwaka 1986 baba yangu na mama hawakuwa wamekutana hivyo sikuwa hata kwenye mpango ila najisikia kuchoka kuliko hao waliokuwepo kabla yangu #pichaza1986 unaugusa moyo wangu