Leo ni #Jumanne ya Kutoa—Changia Global Voices

GV_GivingTuesday2

Leo ni #JumanneyaKutoa, siku maalum kwa kuonesha ukarimu wa kila namna duniani kote. Makala iliyoandikwa na mwanachama wa familia ya Global Voices mwenye asili ya Lebanoni Joey Ayoub masaa machache baada ya shambulio la Paris inatukumbusha jambo hili, na sababu ya sisi wa Global Voices kufafanya kile tunachokifanya.

Katika makala ya Mitaa ya Paris Inavyonikumbusha Mitaa ya Beirut, Joey anaandika kwa ustadi kuhusu “kushindwa kwa sisi binadamu kujitazama kwa sura ya usawa.” Anaongeza:

“Ni vigumu kuelewa kwamba kwa yote yaliyosemwa, kwa maneno matupu tuliyoweza kuyatamka kwa jina la ‘mshikamano na wahanga’, wengi wetu tulio binadamu kama wengine tunatengwa na kelele hizi hewa za mshikamano wa kile kinachoitwa ‘dunia’”

Kila siku katika Global Voices wahariri na waandishi pamoja na watafsiri wetu wa kujitolea wanafanya kazi kuvuka mipaka ya nchi zao, saa za mahali waliko na kuvuka viambaza vya lugha kukuletea habari zinazotokana na sauti za wananchi wa kawaida ambazo kwa kawaida hazithaminiwi sana vyombo vikuu vya habari, kukuleta taarifa za uhuru wa kujieleza mtaoni na kuwaunga mkono wale wote wanaoungana na majadiliano haya ya mtandaoni.

Ili kuendelea kuwa na huru na kufanya kazi zetu ziwe endelevu, tunategemea misaada ya marafiki na wasomaji wetu kama wewe. Mchango wako utatusaidia kulipia gharama za kuwa mtandaoni, gharama za uendeshaji, miradi midogo ya ufadhili na wafanyakazi wa Global Voices.

Katika siku hii ya #Jumanne ya Kutoa, tafadhali fikiria kutuunga mkono sisi wa Global Voices kwa kutoa mchango.

Au kama wewe hufanya manunuzi kwa njia ya Amazon, bonyeza kiungo hiki kabla ya kufanya manunuzi yako, na Amazon Smile watatoa kiasi kidogo cha bei uliyonunulia bidhaa kwa Marafiki wa Global Voices.

Shukrani nyingi sana kutoka familia ya Global Voices!

GT_logo2013-final1-1024x85

Changia sasa »

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.