- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanablogu wa Zone9 Wasema, ‘Kushikiliwa kwetu Kumefunua Yaliyojificha Nchi Ethiopia’

Mada za Habari: Ethiopia, Censorship, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, GV Utetezi
Zone9 bloggers, together after their release. Photo via Zone9 Facebook page.

Wanablogu wa Zone9, wakiwa pamoja mara baada ya kuachiwa huru. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Zone9.

Mara baada ya kukutwa bila ya hatia na kisha kuachiwa huru kutoka gerezani, Wanablogu wa Zone9 kutoka Ethiopia [1] wametoa tathmini kwa yale yaliyowakuta pamoja na kuwashukuru wote waliowaunga mkono. Wanablogu hawa waliwekwa kizuizini April, 2014 na kisha kushtakiwa chini ya sheria ya nchini Ethiopia ya kupambana na ugaidi. Wanablogu watano wa Zone9 waliachiwa huru mwezi Julai, 2015 na wengine wanne waliokuwa wamesalia hawakukutwa na kesi ya kujibu na hivyo kuachiwa huru wiki ya tarehe 19, Oktoba, 2015. Jifunze zaidi [1] kuhusu shitaka lao.

Mkala hii iliandikwa kwa ushirikiano wa Zone9 [2] na kutafsiriwa na Endalk Chala [3] kutoka lugha ya Kihabeshi kwenda katika lugha ya Kiingereza.

Kuachiwa kwetu huru kulikuwa kwa kushangaza kama ilivyokuwa kushikiliwa kwetu. Watano miongoni mwetu waliachawa huru mara baada ya mashtaka yao “kufutwa” mapema mwezi Julai. Wanne tuliosalia tualiachiwa huru mapema mwezi Oktoba kwa kuwa hatukukutwa na kesi ya kujibu (hali iliyotuwezesha kukosekana kwa ushahidi dhidi yetu). Bado kuna mmoja wetu, Befeqadu, ambaye aliachiwa kwa dhamana na anapaswa kuwasilisha utetezi wake mwaka huu mwezi Disemba. Pamoja na kuwa tuliachiwa huru kwa sababu tofauti tofauti, kuna jambo moja linalotufanya tushabihiane- Imani yetu thabiti kwamba, hatukustahili kutiwa kizuizini hata mara moja.

Ndio, ni vizuri kuachiliwa huru, lakini hatukustahili kutiwa kizuizini. Tulichokifanya kilikuwa ni kuandika na kupigania utawala wa sheria kwa kuwa tunahitaji uboreshwaji wa nchi pamoja na maisha bora kwa raia. Hata hivyo, kuandika na kuwa na ndoto ya Taifa bora ilitupelekea kutiwa kizuizini, kudhalilishwa, kuteswa na kuishi mbali na nyumbani. Haikustahili.

…kuandika na kuwa na ndoto ya Taifa bora ilitupelekea kutiwa kizuizini, kudhalilishwa, kuteswa na kuishi mbali na nyumbani. Haikustahili.

Tunafurahi pale tunaposikia kuwa watu wanatiwa hamasa kwa kupata habari zinazotuhusu. Hata vivyo, tunajisikia vibaya pale tunapotambua kuwa watu wanaogopa kuandika kwa kuwa wameshuhudia masahibu tuliyopitia kwa sababu ya kuandika kwetu. Kufungwa gerezani kumetufanya tuwe na furaha pamoja na hofu kuu kwa wakati mmoja. Jambo la muhimu kabisa ni kuwa, ni vizuri kufahamu kuwa tumewapa watu hamasa na kwa upande mwingine inahuzunisha kuwa watu wameacha gumzo kubwa miongoni mwa raia kufuatia kushikiliwa kwetu gerezani. Inahuzunisha kufahamu kuwa kushikiliwa kwetu kulipelekea hali kukata tamaa miongoni mwa raia.

Sisi ni wahanga wa kukosekana kwa uwajibikaji wa makusudi. Lakini hili halipo mbali na uwezo wetu wa kusamehe. Kwa wale waliotufunga gerezani na ambao walitusababishia madhila haya, hata kama hautuombi msamaha, sisi hatuna kinyongo.

Kushikiliwa gerezani kulitufanya kujisikia kuwa maisha yetu hayakuathiriwa. Nni kweli kuwa tulikosa vingi na kupoteza vingi. Lakini pia, tumeongeza wigo wetu wa kujifunza. Tumejifunza mengi sana. Kushikiliwa kwetu gerezani kumetupa simulizi pana sana kuihusu nchi yetu. Tumeweza kushuhudia gharama ya uhuru wa kujieleza kwa namna iliyotugharimu kupita kiasi. Sisi ni mashuhuda halisi wa kunyimwa haki. Kubwa kuliko yote, tumejifunza kuwa taifa lililo kithiri kwa uminywaji wa haki ndilo adui nambari moja kwa raia wanaofuata sheria.

Sisi ni wahanga wa kukosekana kwa uwajibikaji wa makusudi. Lakini hili halipo mbali na uwezo wetu wa kusamehe. Kwa wale waliotufunga gerezani na ambao walitusababishia madhila haya, hata kama hautuombi msamaha, sisi hatuna kinyongo. Tunawaomba mtusamehe, kwa kuwa, sisi ni raia tunaofuata sheria na ambao tunakataa kuishi kwa kufuata matakwa yako.

Kwa watu wote ambao walikuwa nasi wakati wa shida na raha, wale waliokuwa nasi wakati wote siyo tu wa mafanikio bali hata pale tuliposhindwa, NINYI ni watu wazuri!Ninyi ni marafiki wetu, ninyi ni familia yetu, mlikuwa wanasheria wetu, mlitupigania, na mlitulinda. Tunasema asante! Mashirika ya habari, makundi ya haki za binadamu na wanaharakati pamoja na jamii yote ambayo iliungana nasi katika hali tulizopitia. Tunashukuru! Nyote mnastahili pongezi za dhati kabisa kwa kila mlilolifanya kwani lilipunguza muda wetu wa kukaa gerezani pamoja na kutupunguzia hali ya kukata tamaa katika kipindi tulichokuwa gerezani.