- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Sassou-Nguesso Aungana na Marais Wengine wa Maisha Barani Afrika

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Jamhuri ya Kongo, Haki za Binadamu, Maandamano, Mahusiano ya Kimataifa, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala
Dennis Sassou Nguesso via wikipedia CC-BY-20 [1]

Dennis Sassou Nguesso. Picha kupitia ukurasa wa Wikipedia CC-BY-20

Mnamo Novemba 6, Rais wa Jamhuri ya ki-demokrasia ya Kongo, Denis Sassou-Nguesso alijipatia ushindi katika kura ya maoni iliyokuwa iamue ikiwa angeweza kugombea Urais kwa mara nyingine, kufuata nyayo za watawala wenzake wa Rwanda, Burundi na Jamhuri ya ki-Demokrasia ya Kongo (DRC), ambapo ma-Rais waliodumu madarakani kwa muda mrefu wanajaribu kubadili katiba zao ili kujiongea muda wa kubaki madarakani.

Kura hiyo ya maoni ilipigwa vikali na vyama vya upinzani nchini humo na kusababisha vifo kadhaa katika maandamano yaliyoendelea kwenye baadhi ya mitaa ya makao makuu ya nchi hiyo, Brazzaville, wakati wa juma la kuelekea kura hiyo iliyofanyika Oktoba 25.

Sassou-Nguesso alikuwa rais wa Jamhuri ya Watu wa Kongo kati ya 1979 na 1992 na aliendelea kushikilia madaraka hata baada ya nchi hiyo kubadili jina na kuitwa Jamhuri ya Kongo kuanzia mwaka 1997.

Manifestations #Sassoudegage via kabolokongo.com [2]

Maandamano ya #Sassoudegage. Picha kupitia kabolokongo.com

Mapigano wakati wa maandamano ya kupinga kura hiyo ya maoni  

Katiba ya Jamhuri ya Kongo (nchi inayofahamika pia kama Kongo-Brazzaville) inamzuia rais kutawala zaidi ya vipindi viwili, na imeweka umri wa mwisho wa rais kuwa madarakani ambao ni miaka 70.

Mwanzoni mwa 2015, Sassou-Nguesso aliandaa mfululizo wa mashauriano na baadhi ya watu muhimu kisiasa nchini humo ili kuangalia uwezekano wa kurekebisha katiba ambayo imekuwa ikitumika tangu mwaka 2002.

Mpango huo ulikosolewa vikali na wapinzani wake, walioutafsiri kama mchezo wa rais aliyepo madarakani kufanya jaribio la kutaka kugombea kwa muhula wa tatu.

Sassou-Nguesso, hata hivyo, aliendelea na mpango wake na kuitisha kura ya maoni, akiwauliza wananchi wa Kongo kama wanaweza kubariki marekebisho yanayoweza kumwezesha kubaki madarakani.

Kabla ya kupigwa kura hiyo, vyama vya upinzani vilitangaza kususia zoezi hilo, na maandamano yalilipuka kumpinga rais katika miji kadhaa, hususani Brazzaville na Pointe-Noire.

Mamlaka zinasema  watu wanne walipoteza maisha na 10 wengine walijeruhiwa [3] katika mapigano wakati wa juma la kura hiyo ya maoni kama alama habari za #Sassoufit [4] (inayochezea jina la ukoo la rais huyo na kulichanganya na neno la Kifaransa lenye maana ‘imetosha’) na #Sassoudegage [5] (Sassou nje) zikitumika sana kwneye mitandao ya kijamii.
Pamoja na watu kujitokeza kwa kiwango kidogo cha asilimia 10 [6] kura hiyo ya maoni hata hivyo iliidhinisha ushindi wa ‘ndio’, na hivyo kutengenezea njia ya mabadiliko ya katiba aliyoyataka mhe. Sassou-Nguesso.

Mots clefs #sassoufit lors des manifestations contre Nguesso via canalfrance info [7]

kauli mbio za #sassoufit kwenye maandamano yanayompinga Nguesso. Picha kupitia canalfrance info

Nini Mustakabali wa Kongo-Brazzaville? 

Kwa vyama vya upinzani, idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura ni ishara ya ushindi na umaarufu wake kuhusu suala hilo la mabadiliko ya katiba.

Ismaël Bowend Nabole, mwandishi wa Omega FM iliyopo jijini Brazzaville, anasema kwamba vyama vya upinzani nchini humo viliyakataa [8] matokeo hayo:

Une des deux principales plateformes de l’opposition a qualifié le référendum de « coup d’État constitutionnel », car « le scrutin n’a été ni libre, ni juste, ni équitable, ni transparent » et s’est déroulé « dans un état de siège ».

Vyombo viwili vikuu vya habari vinavyomilikiwa na vyama vya upinzani vimeita kura hiyo ya maoni “Mapinduzi ya kikatiba” kwa sababu kura hiyo haikuwa huru, wala haki, ilijaa upendeleo bila uwazi” na ilifanyika “katika mazingira ya utekaji”.

Jumuiya ya kimataifa na waangalizi wa uchaguzi wamekuwa na wasiwasi na matokeo hayo [9].

Michel Taube, Mkurugenzi wa tovuti ya habari inayotumia lugha ya Kifaransa “l'Opinion Internationale” alielezea upinzani wa serikali ya Ufaransa [10] kuhusu uchaguzi huo:

François Hollande, président de la République française, lâche Denis Sassou-Nguesso. Dans un communiqué tardif, après des propos tenus la veille qui avaient déçu toute l’Afrique, l’Elysée « condamne toute violence et soutient la liberté d’expression. [François Hollande] rappelle qu’il avait souhaité, lors de son discours prononcé à Dakar, le 29 novembre 2014, que les Constitutions soient respectées et que les consultations électorales se tiennent dans des conditions de transparence incontestables. » Or il est clair qu’avec son référendum constitutionnel prévu dimanche, Denis Sassou-Nguesso ne respecte pas la Constitution du Congo et n’offre aucune garantie de transparence incontestable.

François Hollande, Rais wa Ufaransa, amejitenga na Sassou-Nguesso. Baada ya kusababisha mshangao kote barani Afrika kwa matamshi aliyoyatoa mbele ya vyombo vya habari siku moja kablda, Elysée ilisema “inalaani ghasia zozote na inaunga mkono uhuru wa kujieleza. [François Hollande] anatoa mfano wa hotuba yake aliyoitoa jijini Dakar mnamo Novemba 29, 2014 alizungumzia matarajio yake kwa katiba zote kuheshimiwa na zoezi la kuwasikiliza wapiga kura kufanyika katika mazingira yenye uwazi wa kutosha.” Sasa ni wazi baada ya kura ya maoni ya Jumapili kwamba Denis Sassou-Nguesso, haheshimu katiba wala kuweka uwazi usio na shaka.

Taube aliongeza kwamba upinzani utailazimisha serikali na vyama vya upinzani kuchukua tahadhari kwa sababu mgogoro wa kisiasa unaendelea kufuka nchini humo:

Rappelons-le : en Tunisie comme au Burkina Faso, quelques heures avant, Ben Ali et Blaise Compaoré ne se doutaient pas qu’ils quitteraient dans la précipitation le pouvoir et que la démocratie l’emporterait enfin sur l’omnipotence d’un seul homme.

Tusisahau: masaa kadhaa kabla ya kung'olewa, Ben Ali wa Tunisia na Blaise Compaoré wa Burkina Faso hawakuwa na habari kuwa demokrasia ingeshinda dhidi ya watawala wanaojiona wana nguvu zote.

Vijana wa nchini hiyo wana matumaini na mustakabali wao, lakini hata hivyo wana wasiwasi mkubwa kwa maslahi ya kisiasa yanayotishia ustawi wa nchi yao.

Wanafunzi watatu, Josué Mfutila Kiangata, Aaron Malu Mukeba na Martin Nomapungu walitoa [11] maoni yao kwenye tovuti ya habari za Afrika inayoitwa Waza Online kuhusu hali yamaono inavyoendelea nchini humo.

Martin:

Certains candidats crient à la victoire avant les élections ; ils insinuent que les dirigeants des institutions chargées d’organiser les élections sont de telle obédience. Or ces institutions doivent être neutres, indépendantes. Cet organe est composé d’hommes politiques ; ils viennent avec leurs tendances politiques.

Baadhi ya wagombea wanadai wameshinda kabla ya uchaguzi; wana maana kwamba wakuu wa taasisi zinazoendesha uchaguzi ni vibaraka wao. Lakini taasisi hizi hazikupaswa kuwa na upande na zilitakiwa kuwa huru. Ni vyombo vilivyoundwa na wanasiasa; vinakuwa na maslahi fulani ya kisiasa.

Aaron:

 je pense que les principes démocratiques sont universels et que nous sommes censés respecter ces principes. Je ne suis pas de ceux qui pensent que le système héréditaire africain d’hier était un bon système.

Ninadhani misingi ya kidemokrasia inafanana duniani kote na kwamba tunapswa kuiheshimu. Sikubaliani na wale wanaofikiri mfumo wa zamani wa ki-Afrika kurithishana ulikuwa mfumo mzuri.

Josué:

La littérature nous enseigne qu’il faut organiser les élections dans un contexte apaisé. Or ici en Afrique, ce n’est pas le cas. Pourquoi ? Parce qu’il s’agit d’une culture empruntée, une culture des Occidentaux qu’on est venue imposer ici en Afrique.

Fasihi inatufundisha kwamba lazima tuandae uchaguzi kubadilisha mambo. Lakini hapa Afrika mambo hayaendi namna hiyo. Kwa nini? Kwa sababu ni utamaduni ulioazimwa, utamaduni wa wa-Magharibi ulioletwa Afrika bila kuangalia mazingira halisi.