Kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita, msanii wa Kifilipino Federico Boyd Sulapas Dominguez amekuwa akiandaa picha zinazoonesha harakati za wazawa katika kukomesha uchimbaji madini [2] wa uharibifu, utafutaji maendeleo usiojali haki, pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi. Lengo lake ni kuifahamisha jamii kuhususiana na masaibu yaikumbayo jamii ya watu waishio Ufilipino pamoja na harakati zao za kulinda ardhi waliyorithishwa na mababu zao.
Ufilipino ina zaidi ya wakazi wazawa milioni 14 ambao [3] huzungumza lugha zaidi ya 110 za kikabila. Hata hivyo, urithi huu wa aina yake unahatarishwa na ongezeko la haraka la miji, harakati za kibiashara pamoja na uporaji wa ardhi yao kupitia shughuli zinazopewa baraka zote na serikali zikiwamo zile za kilimo, uvunaji miti na uchimbaji wa madini.
Katika kisiwa cha Mindanao, kilichopo kaskazini mwa Ufilipino, jamii ya watu wa huko hujulikana kwa jina la lumad. Makundi anuai ya Lumad ambayo yanapinga kuingiliwa na makampuni ya uchimbaji madini yamejitokeza kwenye vyombo vya habari [4] kati ya miezi ya Septemba na Oktoba 2015 mara baada ya kushambuliwa na makundi ya watu mithili ya wanajeshi. Takribani watu 700 wa jamii ya Lumad wameweka kambi [5] jijini Manila, mji mkuu wa Ufilipino, kwa ajili ya kushinikiza kuondolewa kwa wanajeshi kwenye makazi yao.
Malalamiko ya Lumad yanaonekana sana kwenye kazi nyingi za Federico. Amekuwa pia akipakia nakala ya kazi zake za zamani katika ukurasa wake wa Facebook ambazo anaziona kama bado zina manufaa kufuatia kuvamiwa kwa jamii ya Lumad na matukio ya mfululizo ya kurubuni mali asili zilizopo kwenye maeneo ya urithi ya makabila haya. Baadhi ya michoro yake tayari imeshasambazwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii na wanaharakati, wanazuoni pamoja na watetezi wa masuala ya urithi ambao wanalenga kuhamasisha jamii kusaidia jamii ya lumad kupata haki yao.
Federico, ambaye ni wa kabila la Mandaya (Jamii ya wazawa wa lumad kutoka Mashariki ya Mindanao), anawahamashisha wasanii wachanga kuongeza maaarifa yao kuhusu utamaduni wa Ufilipino kwa kujumuika na jamii za wazawa.
Ifuatayo ni baadhi ya michoro ya Federico: