- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hivi Ndivyo Chechen Inavyokabiliana na Kundi la ISIS

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Syria, Urusi, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana, Vita na Migogoro, RuNet Echo

Chechen leader Ramzan Kadyrov. May 27, 2008. Photo by Sergei L. Loiko. CC 2.0. [1]

Kiongozi wa Chechen, Ramzan Kadyrov akicheza na Chui kwenye hifadhi maalum ya wanyama. Mei 27, 2008. Picha na Sergei L. Loiko. CC 2.0.

Kadiri Moscow inavyojaribu kuimarisha ushiriki wake kwenye vita vya nchini Syria, jamii kubwa ya kimataifa imekuwa ikifuatilia na kujadili kwa ukaribu kuhusiana na azma ya Urusi nchini Syria, wakihoji ikiwa msaada wa Kremlin kwa Rais Bashar al-Assad ni msaada muafaka kwa kampeni ya Magharibi ya kulitokomeza kundi la ISIS, ambayo pia inahusisha na harakati za kumuondoa madarakani Assad. Wakati watu wengine wakihoji kuhusu utayari wa Moscow wa kukabiliana na ISIS nchini Syria, harakati za Urusi dhidi ya kikundi katili cha ISIS nchini humo ni dhahiri kabisa. Mapema wiki hii, iongozi wa Jamhuri ya Kirusi ya Chechnia, Ramzan Kadyrov aliwatahadharisha watu kuhusiana na mazingira halisi ya vita hivi.

Kwenye makala [2] ya Vkontakte (Mtandao wa Kijamii maarufu wa Kirusi), Kadyrov alipakia vido fupi iliyokuwa ikionesha watu takribani nusu dazeni waliokuwa wamesimama kwenye mstari huku wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa aibu. Akiongea kwa lugha ya Kichechnia, Kadyrov anawatambulisha watu hao huku akiwa na taswara mbaya dhidi yao. Na kilichofuata, mwanaume mkongwe na pia mwanamke mkongwe wanaongea na watu hao kwa hasira na huzuni tele. Wanawasema. Wanapaza sauti zao. Wanazificha nyuso zao kwa mikono yao.

Video hii inawaonesha wanaume wa Chechen waliokamatwa kama mawakala wanaotumiwa kusajili wanachachama wapya wa ISIS kupitia mitandao ya kijamii na watu waliokwenda umri wanaowafokea ni ndugu zao pamoja na viongozi wa jamii ya hapo. Pia, Kadyrov anatanabaisha kuwa, taarifa za watu hawa zilifikishwa kwa polisi na ndugu wa familia zao wenyewe.

Я встретился с родственниками молодых людей, выступавших в соцсетях в поддержку Иблисского государства. Также пригласил имамов и глав населённых пунктов. У всех заблудших, уважаемые и глубоко религиозные родители, которые искренне осуждают поступки сыновей. Родители однозначно заявили, что растили сыновей в надежде на то, что они станут опорой в семье, будут истинными мусульманами и достойными гражданами. Они подчеркнули, что им не нужны такие сыновья, предавшие семьи, родных, близких, ислам и народ. Один из юношей искал слабохарактерных, слабоумных ровесников и агитировал выехать в Сирию. Он рассылал сообщения, в которых содержались угрозы представителям власти и их семьям. Я еще раз заявил, что в Чечне нет места тем, кто даже смотрит в сторону Иблисского государства. Самое главное, что родители тесно сотрудничают с духовенством и органами власти. При подозрительном поведении сыновей, они сразу же ставят в известность полицию и глав администраций. Это позволяет предотвратить худшие последствия.

Nilikutana na ndugu wa vijana waliokuwa wakilitangaza kundi la ISIS kwenye mitandao ya kijamii. Niliwaalika pia maimamu kadhaa na viongozi wa kijamii. Watu hawa waliopotoshwa wana wazazi ambao ni waaminifu, waumini wa kweli wa dini wanaowalaumu watoto wao kwa vitendo vyao. Mara kadhaa, wazazi hawa walitanabaisha kuwa waliwakuza watoto wao waje kuwa tegemeo kubwa kwa familia zao, wawe waislam wa kweli na raia wazuri. Walisema pia kuwa hawakuwa na sababu ya kuwa na watoto waliosaliti familia zao, ndugu zao, wapendwa wao, uislam pamoja na watu wao.

Mmoja wa vijana hawa wadogo alikuwa akitafuta wenzake ambao hawakuwa na uwezo mzuri wa kung'amua mambo na kujaribu kuwashawishi waende nchini Syria. Alisambaza jumbe zilizokuwa zikitoa vitisho kwa mamlaka za serikali pamoja na wanafamilia.

Niliwaambia tena kwa mara nyingine: Chechen hakuna nafasi kwa yeyote awaye anayejaribu kujihusisha kwa namna yoyote na ISIS. Jambo la muhimu zaidi ni kuwa wazazi wanashirikiana kwa ukaribu kabisa na viongozi wa dini pamoja na polisi. Mara tu wanapoona kuna dalili zisizoridhisha, kw haraka sana huwajulisha polisi pamoja na maafisa wengine wa eneo husika. Utaratibu huu husaidia pia kuzuia kutokea kwa madhara mengine makubwa yasiyotarajiwa.

Kadyrov anafahamika sana kwa matumizi yake ya mitandao ya kijamii. Ana takribani watu milioni 1.2 wanaomfuatilia kwenye Instagram (ambapo kwa sasa akaunti yake imefichwa kwa watumiaji ambao hawajajisajili) na zaidi ya wafuatiliaji 235,800 kwenye Vkontakte. Kadyrov siyo mara chache amekuwa akichukua video za watu waliokuwa wakikaripiwa na wazazi wao pamoja na viongozi kwa kutuhumiwa kuonesha msimamo mikali ya kiislam. Kwa mfano, Juni 2015, kwa utaratibu uleule alikusanya [3] takribani wanaume wanaokadiriwa kufikia dazeni moja mbele ya wazazi wao waliokuwa wamekasirika kwa kitendo cha wanaume hao cha kushinikiza wanawake wawe wanavaa nguo za kiislam za kufunika mwili wote. (Kwa kawaida, wanawake wa Kichechni huvaa vitambaa vya kichwani lakini siyo vali la kufunika mwili mzima)