- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Fuatilia Uchanguzi wa Kihistoria Kuwahi Kutokea Nchini Tanzania

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi
Former Tanzanian Prime Minister and main opposition presidential candidate Edward Lowassa. Photo by TZA One and released under Creative Commons.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania na Mgombea urais kwa tiketi ya Muungano wa vyama upinzani, Edward Lowassa. Picha na TZA One na imetolewa kwa masharti ya Creative Commons.

Uchaguzi mkuu wa Octoba 25 nchini Tanzania utakuwa na ushindani mkali kuliko uchaguzi mwingine wowote uliowahi kufanyika katika historia ya nchi hiyo baada ya Waziri Mkuu mstaafu na mwenye umaarufu mkubwa, Edward Lowassa kuachana na chama tawala na kujiunga na umoja wa vyama vya upinzani.

Lowassa alikihama chama tawala mapema mwisho wa mwezi Julai mara baada ya kuenguliwa kwenye orodha ya wawania kiti cha urais kupitia chama tawala Chama Cha Mapinduzi [1] (CCM). Muda mfupi baadae, alieleza nia yake ya kujiunga na chama cha upinzani, Chama Cha Demokrasia and Maendeleo [2] (Chadema).

Lowassa anadai kuwa hakutendewa haki na hivyo kukoseshwa nafasi ya kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama tawala. Kwa sasa, amekuwa mgombea pekee wa urais atakayeuwakilisha umoja wa vyama vinavyotetea kupatikana kwa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Ikizingatiwa kuwa Lowassa anaungwa mkono na watu wengi, hususani vijana, hii ni mara ya kwanza katika historia ya siasa ya mfumo wa vyama vingi kwa upinzani nchini Tanzania kuwa na nafasi kubwa ya kushinda nafasi ya kiti cha Urais.

Baada ya kutoka chama tawala, wanachama wengine kadhaa wa kutoka chama tawala wakiwemo wabunge, madiwani na viongozi wengine wa mikoani nao walihamia kwenye chama kikuu cha upinzani, Chadema. Waziri Mkuu mstaafu mwingine, naye alihamia upinzani.

Hata hivyo, kuhama kwake kumeleta mtikitisiko.

Hadi kipindi cha hivi karibuni, Chadema ilikuwa ikimuona Lowassa kama fisadi na mtu alisiyeoongozwa na misingi inayoeleweka. Chadema waliongoza mapambano ya kumtaka kuachia madaraka wakati alipotuhumiwa kuhusika kwenye kashfa ya ufisadi iliyomlazimisha [3] achukue uamuzi wa kujiuzulu [4] 2008.

Mara zote amekuwa akikanusha kuwa ofisi yake ilihusika kupokea rushwa ili kuwezesha kupitishwa mkataba mkubwa wa uzalishaji umeme kutoka kwa kampuni ya Kimarekani ya Richmond Development.

Baadhi ya wanachama wa Chadema wameshangazwa na hatua ya chama hicho kumpokea na wamepinga kwa kukihama chama.

Hata hivyo, umaarufu wa Chadema unaonekana kuongozeka mara baada ya kupitishwa kwa Juma Duni Haji [5] kama mgombea mwenza wa Lowassa.

Haji, ambaye katika chaguzi za miaka kadhaa iliyopita amekuwa akigombea kwenye nafasi za kitaifa kwa tiketi ya vyama vya upinzani, alikuwa waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano hadi kipindi Lowassa anaihama CCM.

‘Muda wa Mabadiliko ndio huu’

Umaarufu wa Lowassa ulionekana dhahiri pale alipodhaminiwa na watu zaidi ya milioni 1.5 [6].

Vido ya You Tube ifuatayo inaonesha siku ambayo Lowasa alipochukua fomu ya kugombea urais:

Lowassa alilifanya jiji la Dar Es Salaam kuzizima [7] wakati alipokwenda kuchukua fomu ya kugombea urais. Wakati pekee ambao Dar es Salaam ilishuhudia umati mkubwa wa watu ni wakati wa ziara ya Raia wa Marekani Barack Obama alipozuru nchi hiyo mwaka 2013.

Mitandao ya kijamii imekuwa na mijadala mikali yenye hamasa kubwa. Kama chaguzi zingefanyikia kwenye mtandao wa Twita, matokeo yangekuwa kama inavyotabiriwa.

Albert Gasper Msando alimfananisha Lowassa na Robin Hood [10] na El Chapo [11]:

Lowassa ni Robin Hood wa Kimasai. Au ni El Chapo wa kitanzania. Tazama mikono aishikayo na siyo vidole avikanyagiavyo

Mwamfupe Anyisile alitoa ushauri kwa chama tawala:

Given Edward ana matarajio:

Kama uchaguzi utafanyika leo, nina uhakika kuwa Lowassa anashinda

4 Samaritan Lepers aliielezea haiba ya Lowassa:

Lowassa ni aina ya mtu ambaye “akikukuta” uliko, unasahau ulichokuwa unakifanya. Anakuangalia na kisha anakwambia, “NIFUATE”

DirectoR NiCKLASS aligusia hisia zinazoambatana na wanachama wa Chadema kuvaa magwanda:

Akijibu hoja kuwa Chadema bado hakijawa na uzoefu wa kutosha wa kuongoza nchi, Edward Lowassa alijibu mwenyewe kwa kusema:

Isack Danford alitwiti:

Uasi wa jamii. Mabadiliko yanatokea. CCM watoke kabisa, siwapendi na siwezi kudanganya

Mwamfupe Anyisile alionesha atapigaje kura yake:

Mwacheni Lowassa awe rais wa Tano wa Tanzania

And Leylah Malweezy anaamini kuwa Lowassa anasaidiwa na nguvu za Mungu:

George Roberts aliweka picha inayoonesha namna ya kipekee ya Chadema ya kujitambulisha kwa wapiga kura:

Chama cha upinzani kikitumia kila njia ili kujitambulisha kwenye mkutano wao wa kampeni leo huko Mbeya

Hata hivyo, siyo kila mmoja anayemuunga mkono Lowassa na Chadema.

Akijibu maoni ya Musa Kilembo, kwamba Lowassa amekubalika kwa wapiga kura,  Evarist Chahali alisema:

Hata mimi pia. Siyo tu kuwa nilikuwa ninapambana na maovu yafanywayo na CCM, lakini pia nilijitolea kwa dhati sana. Hata hivyo, sina imani na Lowassa kama mbadala

Suphian Juma hamuamini Lowassa:

Asili hata siku moja haiachi ombwe. Tuna hakika gani kuwa wewe upo kinyume kabisa na CCM?

Bernard Matungwa aliandika:

Malengo makuu mawili ya Chadema, La kwanza: Kufanya CCM kuwa chama cha upinzani. La pili: Kuipora nchi! Inatisha. Inatisha kabisa!

Nathaniel Imani alidokeza kidogo kuhusiana na yaliyomkuta Lowassa kipindi cha nyuma:

Pia, Hamisi Kigwangalla ana matumaini kuwa Chama tawala, CCM kitahimili mikikimiki ya sasa:

Watu wapya ndani ya CCM watakijenga tena chama na serikali, na hapo upinzani utajifia kifo cha asili