Edom Kassaye: Mwandishi wa Ethiopia Aliyefungwa Gerezani kwa Uwajibikaji Wake

Edom Kassay. Photo courtesy of Endalk Chala.

Edom Kassaye akiwa kwenye safari ya kitafiti huko Harar, Ethiopia, Julai 2013. Picha na Endalk Chala.

Mnamo mwezi wa Aprili, wanablogu tisa pamoja na waandishi wa habari walikamatwa nchini Ethiopia. Baadhi ya wanaume na wanawake hawa walikuwa wakifanya kazi na Zone9, blogu ya ushirika iliyokuwa inazungumzia masuala ya kijamii na ya kisiasa nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa haki za binadamu na uwajibikaji wa serikali. Miongoni mwao, wanablogu wanne walikuwa ni waandishi wa Global Voices. Mapema mwezi Julai, walishitakiwa chini ya tamko la wazi la nchi dhidi ya ugaidi. Wamekuwa gerezani tangu wakati huo na kesi yao hivi karibuni ndio imeanza kusikilizwa.
Makala hii ni mfululizo wa makala zetu za – “Wanayo Majina” – iliyo na madhumuni ya kuwazungumzia wanablogu ambao hadi sasa wapo gerezani. Tunataka kutambua utu wao, tunataka kuelezea habari zao za kipekee na mahususi kabisa. Simulizi hii inatoka kwa Endalk Chala, mmoja wa waanzilisji wa muungano wa wanablogu wa Zone9 ambaye aliponea chupuchupu kukamatwa kwa sababu zilizotajwa kuwa alikuwa nchini Marekani, anasomea shahada ya Uzamivu ya masuala ya habari.

Nilitokea kumfahamu Edom Kassaye kupitia kwa Befeqadu mwenyekiti shupavu wa jumuia ya wanablogu wa Zone9. Kwa mara ya kwanza tulikutana mwaka 2012, mara tu baada ya yeye kurejea baada ya shughuli yake ya mwaka mmoja ya kuripoti akiwa nchini Kenya. Simulizi alizonipa pamoja na uhuru wa habari alioushuhudia nchini Kenya uliibua majadiliano ya kina kuhusu hali tete ya uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia. Tokea hapo, hadi nilipoondoka nchini Kenya mwaka 2013, mimi na Edom tulikuwa tukikutana mara kwa mara kwa ajili ya kupata kahawa. Tulitokea kuwa marafiki wazuri.

Ninapotafakari muda niliokuwa pamoja na Edom, ninatambua kuwa haishangazi kuona alikamatwa pamoja na wanablogu sita wa jumuia ya Zone9. Watu wanajiuliza ni kwa nini Edom alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la ugaidi ilhali hakuwa mmoja wa wanaounda kundi la Zone9. Ninaamini kuwa ilikuwa nidhamira chanya ya Edom ya kuleta mageuzi sahihi ya siasa hafifu ya Ethiopia ambayo pia ilipelekea yeye kuwa karibu zaidi na wanajumuia wa kublogu wa Zone9. Taratibu zetu ziliwiana.

Edom alishiriki kwenye kila kampeni ya mtandaoni ambayo jumuia ya kublogu ya Zone9 ilishiriki. Inaonekana kuwa, ushiriki wake kwenye kampeni za mtandaoni ndio uliomfanya kufahamika kwake na mamlaka ya nchi ya kufuatilia mitandao ya kijamii. Katika siku na majuma machache kabla ya kukamatwa kwake, Edom alikataa maombi ya kutumiwa kama mtoa taarifa zilizowahusu marafiki zake wa jumuia ya wanablogu wa Zone9. Badala yake, alichagua kufungwa gerezani pamoja na marafiki zake. Uadilifu wake na msimamo wake unaonesha kitu fulani cha pekee alichonacho- utayari wake thabiti katika uraia imara wa jamii ya watu waliorubuniwa na kuparaganyika.. Jomanex, mwanablogu aliye uhamishoni, mwenzake na rafiki yake, mara nyingi hupenda kumwita Edom  ‘ Mrembo Mwadilifu’.

Mahi & Edom2

Edom (kushoto) akiwa na Mahlet akisindikizwa kwenye chumba cha mahakama ndani ya viunga vya Mahakama kuu jijini Addis Ababa. Picha kwa hisani ya Blogu ya ufuatiliaji wa kesi.

Edom ni mmoja wa waandishi wanawake wachache sana ninaowafahamu nchini Ethiopia waliokuwa wanajihusisha na uandishi wa habari katika majukwaa anuai. Wasifu wake unatanabaisha kuwa yeye ni mwandishi anayekua kwa kasi akilenga zaidi kwenye masuala ya mazingira, afya ya jamii na usawa katika jamii. Kwa wasiomjua, Edom alichorwa kama mwandishi chipukizi aliyekuwa na hamasa kubwa na ambaye kazi zake zilionekana takribani kila mahali kuanzia kwenye gazeti la kila siku linalomilikiwa na serikali hadi kwenye vituo vya redio vinavyojitegemea vya Addis ababa. Lakini, maelezo machache tu yanamfanya kuwa tofauti.

Edom alianza kazi yake ya uandishi wa habari akiwa na gazeti la kila siku linalomilikiwa na serikali. Akifanya kazi kama mwandishi wa habari mwandamizi, alijaribu kuonesha msimamo wake kwenye uandishi habari ulio na ubora ambao vyombo vya habari vinavyomilikiwa na taifa la Ethiopia havikuwahi kuuonesha. Hata hivyo, utaratibu wake wa kuuliza maswali ya kiudadisi haukuendana na utamaduni wa uandishi wa kuilinda serikali na ndipo alipoamua kuangalia jambo jingine la kufanya. Mwaka 2011, alifanikiwa kupata nafasi ya kusoma nchini Kenya, ambapo alielekeza nguvu zake kwenye uandishi wa habari za mazingira. Aliporejea, aliamua kutokufanya kazi na vyombo vya habari vya serikali, badala yake, aliamua kufanya kazi na mashirika mbalimbali ya habari kama mwandishi huru. Tulipoanzisha jukwaa la Global Voices’ katika lugha ya Kihabeshi mwaka 2012, yeye alifanya kazi ya kujitolea kama mtafsiri wa tovuti ile. Mwaka 2013, Edom, Befeqadu, Zelalem pamoja na mimi tulifanya kazi ya pamoja ya kuandaa Taarifa ya hali ya Uhuru wa Kujieleza nchini Ethiopia ambayo baadae iliwasilishwa kwenye Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Bidamu kwa ajili ya Mapitio yao ya Jumla ya Mara kwa Mara.

edom_kassaye (2) (1)

Edom Kassaye. Mchoro na Melody Sundberg.

Mwaka 2011, serikali iliwatia kizuizini na kuwashitaki waandishi wa habari zaidi ya 12 kwa makosa ya kigaidi ya kutengenezwa, matukio yaliyokuwa yanaendelea tangu mwaka 2005. Edom aliona ni heri kujitoa na kuungana na wanahabari hawa. Mara kwa mara alikuwa akienda gerezani kwa ajili ya kuwasabahi waandishi na washindi wa tuzo kama vile Reeyot Alemu na Eskinder Nega, ambao hadi sasa wanatumikia kifungo chao kirefu gerezani. Utaratibu huu ulimpa Edom taswira ya hali halisi ya maisha wanayoishi wanahabari hawa wakiwa gerezani. Kama ishara ya kuwaunga mkono wanahabari hawa, mra kwa mara alikuwa akitwiti idadi ya siku ambazo wanahabari hawa walipaswa kuzitumikia gerezani. Nawaza kama kuna siku aliwaza kuwa kuna siku naye angekuwa gerezani kama ilivyo kwa marafiki wake.

Nilimuuliza alipata wapi ujasiri wa kutumia ukurasa wake wa twita kama namna ya kufuatilia muda wanaopaswa kutumikia wanahabari hao wakiwa katika hali mbaya ya maisha ya gerezani. Aliniambia kuwa, katika gereza la Kality, mahali ambapo Eskinder Nega anaposhikiliwa, walinzi huwa wana utaratibu wa kuwahesabu wafungwa kwa kutumia filimbi za asubuhi. Huwa wanapaza sauti sana– ‘Kotera፣ Kotera፣ Kotera’ Ikiwa na maana kuwa, jitokezeni wenyewe kwa ajili ya kuhesabiwa, kwa ajili ya kuhesabiwa, kwa ajili ya kuhesabiwa. Utaratibu huu unatumika kwa magereza yote nchini Ethiopia. Mfumo huu una malengo mawili: kwanza ni kuwafanya wafungwa waamke mapema; na sababu ya pili ni kuwaona wafungwa kwa ajili ya kuhesabiwa. Kwa uchungu, Edom alijijengea utaratibu wake wa kuhesabu katika twits zake kama namna ya kuhesabu siku walizofungwa wanahari wenzake. Edom aliendelea kufanya hivi hadi pale naye alipoungana na wenzake gerezani.

Tangu tarehe 25 Aprili, 2014, Edom alipokonywa haki zake za kutwiti kwa ajili ya kuonesha mshikamano wake kwa wanahabari wenzake waliokuwa wamefungwa gerezani. Kwenye jarida lake la gerezani, ambapo alielezea mazingira ya kukamatwa kwake, aliandika:

ወዲያው ልሂድ ብሎ ወጣ ጣፋጭ በር ላይ ተሰነባበትን ፡፡ ወዲያው አስፓልቱን ስሻገር አንድ መኪና መንገድ ዘጋብኝና ሁለት ተራ ወንበዴዎች የመሰሉ ሰዎች አንድገባ አዘዙኝ፡፡ አልገባም አልኩኝ ፡፡አንደኛው እጄን ጠምዝዞ አስገድዶ ወደመኪናው መራኝ ያኔ መከራከሩ እንደማያወጣ ገባኝ፡፡ ከኋላ አስገብተውኝ ግራና ቀኝ ተቀመጡ፡፡ መኪናዋን ይኸው የትምህርት ቤት ወዳጄ ይዟት እንዳየሁ አስታወስኩ፡። ቆሻሻና ዳሽ ቦርድ የሌላት መኪና ናት፡። ከነሹፌሩ የቀን ስራ ሲሰሩ ውለው ያላባቸው የሚመስሉ ሶስት ወጣቶች አሉ፡፡ ጋቢና ያለው ወጣት “ኤዲ አንዴት ነሽ ?” አለኝ ጸጥ አልኩኝ፡፡ ፓሊስ ጣቢያ ለጉዳይ አንደፈለጉኝ እና ቶሎ አንደምለቀቅ ተናግሮ ሊያረጋጋኝ ሞከረ፡፡ ሹፌሩ ያለምንም ማቅማማት ጥቁር አንበሳ እና ባንኮዲሮማ ህንጻ ጋር ያሉትን መብራቶች እየጣሰ ጉዞ ወደፒያሳ ሆነ፣ ምን እነዳጣደፈው እንጃ ።። ቤተሰቦቼ ጋር አንድደውል ይፈቀድልኝ ብልም ስልኬን ወስደው ፍቃደኛ ሳይሆኑ ቀሩ ፡፡ ማአከላዊ ስንደርስ 12.50 አካባቢ ሆኗል፡፡ መደበኛ ምዝገባ ተደርጎልኝ ንብረቶቼን አስረከብኩ ፣ እርቃኔን ከሆንኩ በኋላ ቁጭ ብድግ እያልኩ ሰውነቴ ሁሉ ተፈትሿል፡፡ ከታሰሩ ሴቶች ጋር ስቀላቀል እራትና የሌሊት ልብስ ሰጡኝ፡። ከጥቂት ሰአታት በኋላ የእግር ኮቴ ስንሰማ ተሽቀዳድመን በቀዳዳ ስናይ ማህሌትን ወደ ሌላ ክፍል ሲያስገቧት አየሁ ፡፡ ያኔ ለመጀመሪያ ጊዜ አለቀስኩ ፡፡ ቤተሰቦቼ ልጃችን ምን ዋጣት ብለው አንዴት አንደሚነጋላቸው እየተጨነኩ ነጋ፡፡

Nilipokuwa ninavuka barabara, gari lilikuja na kunizibia njia. Wanaume walioonekana wakatili walinivamia na kisha kunilazimisha kuingia kwenye gari. Nilipokataa kuingia garini, mmoja wa watu wale alinikunja kiganja cha mkono; na ndipo nilipogundua kuwa kujaribu kukwepa kukamatwa kusingekuwa na manufaa, hata hivyo walitumia nguvu kunifanya niingie kwenye gari na kisha katika siti ya nyuma, wanaume wawili walikaa kulia na kushoto kwangu. Nikiwa nimekaa huku nikitafakari kimya kimya, niliwaomba waniruhusu niongee na familia yangu. Walinikatalia na kuharibu kikatili simu yangu…. Karibu jua kuzama, tulikaribia Maekelewi, Ushirika wa Kituo cha Upelelezi wa Polisi kinachojulikana kwa ukatili uliopitiliza. Nilipitia kwenye ukaguzi ambao haukuwa wa kibinadamu kabisa kabla ya kupelekwa kwenye sero iliyokuwa na giza ili kuungana na waliokuwemo humo….  Baada ya muda kidogo, tulisikia mtu akitembea na ndipo sote tulikusanyika na kuchungulia kupitia kwenye kauwazi kadogo ili kujua kilichokuwa kikiendelea, nilipomuona Mahlet akipelekwa kwenye sero nyingine…. Katika hali ile, nilipata hisia kali ya kuogopesha kuhusu familia yangu kwani lazima walikuwa kwenye dibwi la hofu ya wapi nilikuwa, hapa nilijikuta nikitokwa na machozi.

Edom amejihusisha na uandishi wa habari ambao pamoja na kuwa uliambatana na kupuuzwa kwa uanaharakati wake, uanahabari wake umekuwa wa kukumbukwa na wa aina yake ya kipekee. Alikuwa akitumia upole wake wa kipekee wa kuwasilisha kile alichokiamini bila ya vitisho wala kuficha ukweli. Miezi miwili kabla ya safari yangu ya kwenda Marekani kwa ajili ya masomo ya uzamivu, Edom alikuwa na safari ya Tunisia, na aliporudi, aliniletea zawadi ya kishikio cha funguo kilichokuwa na mfano wa mchikichi ambao huaminiwa kutoa ulinzi dhidi ya mabaya. Inaniuma sana kwani sikuweza kumpatia Edom ulinzi dhidi ya serikali yetu dhalimu. Ninathamini sana kila dakika niliyoitumia nikiwa na Edom, mwanamke ambaye kwa weledi mkubwa amekuwa akitetea kile alichokiamini.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.