- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanawake Wanaovaa Nusu Uchi Wataiokoa Sekta ya Utalii Kenya?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Safari, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Je, kutembea uchi [1] yanaweza kuwa mbinu bora ya kufufua sekta ya utalii nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabaab?:

Seneta mteule, Mbura anasemekana kuwaomba wanawake katika mkoa wa pwani kutembea nusu uchi ili kuwavutia watalii zaidi kuzuru eneo hilo. Wito huo umeibua maswali kuhusiana na thamani ya mwanamke wa pwani. Je, ndicho anachostahili kuwa – chombo cha biashara?