- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Raia wa Uganda Wanataniana kwa Mgogoro ‘wa Kawaida’ wa Awamu ya Tatu Burundi

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Burundi, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
Burundian president Pierre Nkuruzinza. Photo released under Creative Commons by the World Economic Forum.

Rais wa Burundi Pierre Nkuruzinza. Picha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na World Economic Forum.

Jaribio la Pierre Nkurunziza [1] Rais wa Burundi kujiongezea muhula mwingine wa madaraka [2] lilisababisha maandamano na baadae mapinduzi ya kijeshi [3] mnamo Mei 13, 2015 wakati akiwa kwenye mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Tanzania. Mapinduzi hayo yalimchelewesha kurejea nchini Burundi.

Jumla ya nchi 18 za ki-Afrika [4] hazina ukomo wa mihula ya urais, ingawa utafiti mpya unaonesha [5] kwamba wa-Afrika wengi wanakubaliana na kuwepo kwa ukomo wa mihula ya urais. Kuwepo kwa wanasiasa wanaong'ang'ania madaraka kinyume na matakwa ya wananchi si jambo la kuchekesha tena, ila kicheko kidogo wakati mwingine kinaruhusiwa na daktari.

Mapinduzi yaliyoshindwa nchini Burundi yamesababisha twiti za kuchekesha, hasa kutoka wa-Ganda ambao rais wao wenyewe anasaka uwezekano wa muhula wa tano [6].

Kemigisa Jacky, mwanafunzi wa uandishi wa habari raia wa Uganda, akirejea madai yanayodaiwa kuwa ya Nkurunziza kwamba Mungu amebariki harakati zake za muhula wa tatu, aliandika:

Lakini nina wasiwasi na kile ambacho Mungu anakuambia sasa hivi Nkurunziza! Labda ni Mungu aliyeruhusu harakati za kugombea muhula wa tatu

Mtumiaji mwingine wa mtandao wa twita MartinAhabwe alimwuliza Nkurunziza:

Mkuu hesabu zako vipi tena, huu ni muhula wa ngapi sasa, wa kwanza, wa pili au bado hata mmoja?

Wengine walitengeneza alama ishara ya #NkurunzizaPlaylist, [10]ambapo walituma vichwa vya nyimbo kwa ajili ya Nkurunziza.

Video ya YouTube hapa chini iliwekwa [11] kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama ishara ya #NkurunzizaPlaylist [10] na Mkandamizaji. Hii ilikuwa kabla Nkurunziza hajarudi Burundi kutokea Tanzania kufuatia mapinduzi. Wimbo wenyewe ni ule wa “I Am Coming Home” ulioimbwa na Morgan Heritage:

Allan Ssenyonga, mwalimu na mwandishi wa Uganda, alichagua wimbo wa mwimbaji marehemu wa miondoko ya kufoka foka Tupac Shakur:

Niko kinyume na ulimwengu wote -2pac (Nkurunziza anaonekana mkono wa kuume)

Mtumiaji wa mtandao wa Twita kutoka Uganda Ellis Ralph alipendekeza wimbo wa Tyrese:

Utafanyaje hivyo – Tyrese

Odokonyero, mwanafunzi wa ufamasia alichagua wimbo wa R.Kelly:

Kama ningeweza kubadili nyakati – R. Kelly

Elizabeth Paulat, mwandishi wa habari wa kujitegemea aishie Kampala, Uganda, alichagua wimbo wa mtunzi wa nyimbo Mwingereza Imogen Heap [17]:

HA! Inafurahisha!

@mmnjug alichagua ule wa mwimbaji wa Kiingereza Mark Morrisson [20]:

Kurudi kwa Mack!

The Royco Guy alihisi Nkurunziza amekwama Tanzania huku na suti moja tu:

Unapokuwa umekwama Tanzania na una suti moja tu

Akafikiri Hoteli ingemhudumiaje akiwa “Rais wa zamani”:

Meneja wa Hoteli hapo Dar es Salaam akikuomba kuondoka kwenye chumba cha watu maarufu (VIP) kwa sababu chumba hicho kimetengwa kwa ajili ya Marais….

Pamoja na mgogoro unaoitafuna Burundi, kicheko bado ni afya.