- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msemo Wa Blogu ya Zelalem Kiberet: ‘Uache Uhuru Uvume’

Mada za Habari: Ethiopia, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, GV Utetezi
Zelalem Kiberet at 25. Photo from Zelalem's blog. [1]

Zelalem Kiberet akiwa na umri wa miaka 25. Picha kutoka blogu ya Zelalem.

Mnamo mwezi wa Aprili, wanablogu tisa pamoja na waandishi wa habari walikamatwa nchini Ethiopia. Baadhi ya wanaume na wanawake hawa walikuwa wakifanya kazi na Zone9, blogu ya ushirika [2] iliyokuwa inazungumzia masuala ya kijamii na ya kisiasa nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa haki za binadamu na uwajibikaji wa serikali. Miongoni mwao, wanablogu wanne walikuwa ni waandishi wa Global Voices. Mwezi Julai, 2014 walihukumiwa [3] chini ya tamko la wazi la nchi dhidi ya ugaidi. Tangu wakati huo, wameendelea kuwepo gerezani, huku shitaka lao likiwa linaahirishwa mara kwa mara.

Makala hii ni ya tatu katika matoleo ya makala zetu za – “Wanayo Majina” – iliyo na madhumuni ya kuwazungumzia wanablogu ambao hadi sasa wapo gerezani. Tunataka kutambua utu wao, tunataka kuelezea habari zao za kipekee na mahususi kabisa. Simulizi hii inatoka kwa Endalk Chala, mmoja wa waanzilishi wa umoja wa Zone9 ambaye alisalimika kwa kutofungwa gerezani kwa kile kinachoelezwa kuwa alikuwa nchini Marekani, anaposomea shahada yake ya Uzamivu.

Kwa mara ya kwanza nilikutana na Zelalem Kiberet mwaka 2012. Nilimfahamu kupitia blogu yake, ambapo alikuwa akiandika kwa kiudadisi na kwa mvuto makala kuhusiana na sanaa, siasa, historia na falsafa.

kwangu mimi, kwa kusoma makala zake zilizohusiana na falsafa pamoja na kupiga soga naye mara kwa mara kupitia Facebook, kamwe hakukuniridhisha, hadi pale nilipoamua kuonana naye ana kwa ana. Kwa kipindi hicho, nilikuwa nikitamani sana kukutana na rafiki zangu wa mtandaoni. Hili ndilo haswa hatimaye lililotupelekea kuanzisha Zone9 [4]. Siku hiyo, alikuwa niBefeqadu ambaye ndiye aliyekuwa mshika dau mkubwa wa umoja huu, aliratibu mkutano wetu. Tulikutana kwenye mgahawa uliojulikana kwa jina la Pizza, katikati mwa jiji la Addis Ababa.

Befeqadu na mimi tuliwasili wa kwanza, na baadae Zelalem alijumuika nasi. Alitusalimu kwa bashasha. Tulikuwa tumekaa kwenye meza iliyokuwa karibu na mlango. Aliagiza kikombe kimoja cha macchiato na kisha tukafanya moja ya mazungumzo mazuri kabisa.

Zelalem alikuwa mhitimu katika Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa na pia alikuwa akifundisha masual ya sheria katika Chuo Kikuu cha Ambo. Nilijiona mwenye bahati sana kwa kutokea kufanya kazi na Zelalem. Kutokana na upeo wake mkubwa, uandishi wa kuvutia, na maaandiko yake yaliyokuwa na mvuto na msimamo wake wa kuidadafua dini, marafiki zake walibadilisha kidogo jina la Zelalem na kuwa jina la mwandishi mashuhuri wa Ufaransa, Zola, ambaye hata Zelalem mwenyewe amekuwa akimsoma kwa shauku kubwa. Upendo wa Zola wetu katika masuala ya falsafa na sanaa unajidhihirisha kwake haswa pale alipolifanya tangazo la utambulisho wa blogu yake kuwa ni picha maarufu ya “Kifo cha Socrates” [5] iliyoandaliwa na Jacques-Louis David.

The Death of Socrates, by Jacques-Louis David. Released to public domain. Image via Wikimedia. [5]

Kifo cha Socrates, na Jacques-Louis David. ilitolewa Released to public domain. Picha kupitia Wikimedia.

Twita za Zola zilizopata umaarufu mkubwa zilitosha sana kumuelezea vizuri miongoni mwa wenzake kiasi kwamba ninadiriki kusema kwamba hadi wakati anatiwa kizuizini, Zola tayari alishakuwa Mhabeshi aliyekuwa akisomwa sana katika mtandao wa Twitter. Ukarimu wake na Twiti zake za hekima ya hali ya juu vilimfanya kuwa mtu ambaye ilikuwa lazima kumfuatilia.

Zola anaweza pia kuandika makala zinazodumu kwa kipindi kirefu. Katika moja ya makala zake za blogu, alitoa dhihaka dhidi ya watu fulani ambao kamwe magazeti ya nchini Ethiopia hayakuthubutu kukanusha. Katika malaka moja ya blogu, iliyokuwa na kichwa cha habari “Namna unavyoweza Kuvumbua Dini yako Mwenyewe – Mwangozo wa Kihabeshi”, [6] aliandika makala ndefu ya dhihaka ya namna ambavyo vipindi kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali na harakati zao za kujaribu kupenyeza mfumo wa kidini wa aliyekuwa Rais wa Ethiopia hayati Meles Zenawi. Aina hii ya maandiko yake ulimuweka Zola katika ungalizi wa karibu uliokuwa unafanywa na serikali ya Ethiopia. Hadi wakati huu, takribani mwaka mmoja akiwa gerezani, Zola anakabiliwa na mashitaka ya kutengenezwa yanayomhusisha na ugaidi ati kwa kuwa tu ni mwanazuoni halisi atumiaye unyenyekevu wake katika ukosoaji.

Katika bango la blogu yake, Zola aliandika ‘Acha Uhuru Uvume’. Kwa kuwa bado yupo gerezani, hatuna budi kudumisha matarajio haya kwa niaba yake.