- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwa nini Tarakimu 64, 89 na 535 Hazipatikani Kwenye Mtandao wa Intaneti China?

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Historia, Uandishi wa Habari za Kiraia

Leo ni Juni 4, maadhimisho ya 26 ya maandamano ya kudai demokrasia ya Tiananmen mwaka 1989 [1].

Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya tarakimu zimepotea kwenye mtandao wa Intaneti nchini China kwa sababu ya udhibiti wa taarifa. Tarakimu hizi ni 64, 89 na 535 —zenye kuunganisha kupata Mei 35, namna maarufu yakukumbuka siku ya Juni 4 [1]. Tarakimu hizo hazitafutiki kwenye tovuti za kutafutia taarifa na haziwezi kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.

Mchora katuni za kisiasa Biantailajiao, kupitia mtandao wa twita, alionesha namna hiyo ya kijinga ya kujaribu kufuta historia:

Kama inawezekana, wanaweza kuifuta kabisa tarehe hii kwenye kalenda.