Kampeni ya Kujipiga Picha Yaongeza Uvumilivu wa Kidini na Kupunguza Ukabila Nchini Myanmar

Myanmar My Friend Campaign

Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa kampeni ya #myfriend.

Kampeni ya kujipiga picha nchini Myanmar imeonekana kukuza kuvumiliana na kuongeza urafiki wakati ambapo kuna ongezeko la matukio ya watu kutukanana, kubaguana na ghasia za kijamii katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Kampeni ya mtandao wa facebook inayoongozwa na vijana kutoka jiji kubwa zaidi nchini humo, Yangon, na ilianza mwezi April kwa kuwaomba watu kujipiga picha wakiwa na marafiki zao wenye dini au kabila tofauti na wao na kuzituma picha hizo kwenye mtandao huo.

Kampeni hiyo inatumia alama habari za #myfriend na #friendship_has_no_boundaries.

Tangu mwaka 2012, kumekuwa na ghasia kubwa kati ya baadhi ya waumini wa dini ya ki-Budha na Waislamu walio wachache katika maeneo ya kati, magharibi,na kaskazini mwa Myanmar, ikiwa ni pamoja na Meikhtila lililo katikati ya Myanmar, ambako nyumba za watu wa jamii za ki-Budha na ki-Islam zilichomwa na maelefu ya watu wakiachwa bila makazi. Vurugu kubwa zaidi ni zile zilizotokea mwezi Oktoba 2012 katika jimba la Rakhine magharibi mwa Myanmar, ambako wa-Islamu wa Rohingya Muslims wamekuwa wakiishi kwenye makambi ya wakimbizi karibu na jiji la Sittwe. Serikali ya Myanmar inawachukulia watu wa jamii ya Rohingya kuwa wahamiaji haramu.

Wakati huo huo, kuna matukio ya kusambaa kwa maneno ya kashfa na kutukanana sambamba na unyanyasaji kwenye mitandao ya kijamii nchini humo, hali inayofanya kuwepo kwa mazingira ya kutokuvumiliana pamoja na ubaguzi wa rangi.

Hapa chini unaweza kuona picha za kampeni ya #MyFriend kuthibitisha kwamba watu nchini Myanmar, hususani vijana, wamekusudia kumaliza chuki kwa kuonesha wanavyoheshimiana na kupendana.

Han Seth Lu, Mwislamu, aliweka picha hii akiwana rafiki yake Mbudha:

Myanmar My Friend Campaign (5)

Mimi ni Mbudha na Rafiki yangu ni Mwislam.
Mie mvulana yeye ni Msichana.
Tunaonekana tofauti lakini tunakubaliana.
Maisha hayadumu, furahia sasa.
Kwa sababu urafiki hauna mipaka.
#MyFriend
#Friendship_has_no_boundaries – tunatafuta amani tukiwa na May Khin

Rody Din, Mkristo, anaweka picha akiwa na rafiki yake Mbudha kutoka Thailand:

Myanmar My Friend Campaign (3)

“Mie Mkristo wa Myanmar na rafiki yangu ni Mbudha wa Thailand

Su Yadanar Myint, Mwislamu, anajisikia fahari/a> kuwa naurafiki na mwenzie m-Sikh [Khalasinga]:

Myanmar My Friend Campaign (4)

Huyu ni Msikh [Khalasinga] na mie Mwislam.
Bado tu marafiki.
Ingawa tuna tofauti zetu,
bado tunazungumzia maoni na imani zetu,
tumezikubali na kuziheshimu
tofauti zetu.
#Myfriend
#Friendship_has_no_boundaries

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.