- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Burkina Faso, Burundi, Naija, Togo, Habari za Hivi Punde, Maandamano, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Uhamiaji na Uhamaji, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vijana, Vyombo na Uandishi wa Habari
Protests in Niamey, Niger via Abdoulaye Hamidou on twitter (with his permission) [1]

Maandamano mjini Niamey, Naija kupitia kwenye ukurasa wa Abdoulaye Hamidou kwenye mtandao wa Twita (kwa ruhusa yake)

Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey [2], Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo. Serikali iliachia ngazi nchini Burkina Faso wakati uchaguzi ukiahirishwa nchini Burundi. Mwezi Mei, wananchi wa Lome waliandamana kupinga matokeo ya urais [3] yaliyompa ushindi rais Faure Gnassingbe aliyeshinda kwa muhula wa tatu.