Pamoja na kutiwa nguvuni kwa maafisa kadhaa wa FIFA kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Wizara ya Sheria ya Marekani, chombo hicho kinachosimamia kandanda duniani kimesema kwamba uchaguzi wake, ambao utaunda baraza la 65 la FIFA, utaendelea kama ulivyopangwa hivi leo. Rais wa FIFA aliye madarakani Sepp Blatter, ambaye ameongoza chombo hicho katika kipindi cha miongo miwili inayodaiwa kugubikwa na ufisadi, rushwa na fedha haramu, anatafuta kuchaguliwa kwa muhula wa tano kwenye baraza la leo. Blatter amegoma kujiuzulu pamoja na kuzungukwa na tuhuma, pamoja na mashinikizo yanayomtaka aachie ngazi.
Unaweza kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ya uchaguzi wa FIFA hapa.