- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Tunayoyajua na Tusiyoyajua Baada ya Jaribio la Mapinduzi Nchini Burundi

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Burundi, Tanzania, Habari za Hivi Punde, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uchaguzi, Vita na Migogoro

Shangwe na vifijo karibu na ikulu ya Rais nchini Bujumbura baada ya kupinduliwa kwa Nkurunzisa.

Kufuatia nia ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu [4]ya Rais wa Burundi aliye madarakani Nkurunziza, Jenerali Godefroid Niyombare alitangaza kwamba utawala uliopo umeangushwa rasmi na kwamba anatwaa madaraka mpaka itakapotangazwa vinginevyo. Serikali ilikanusha mapinduzi hayo kutokea na iliyaita “upuuzi” [5]. Hali bado inaonekana kuwatete nchini Burundi, lakini hapa ni mhutasri wa kile kinachofahamika [6] na kile kisichoeleweka vyema jijini Bujumbura, mji mkuu wa Penelope Starr (kupitia blogu ya UN Dispatch):

Rais Nkurunziza haikuwa nchini wakati mapinduzi yakitangazwa (lakini hakuna anayejua ikiwa amerudi au bado) : Rais alikuwa akihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakati mapinduzi hayo yakitangazwa. Amejaribu kureje kwa ndege jijini Bujumbura lakini haijulikani kama alifanikiwa.

Huu si mgogoro (tu) wa kikabila :

Nkurunziza na Jenerali Niyombare wote walikuwa viongozi wa waasi wa Ki-Hutu. Zote wako kwenye serikali ya chama hicho hicho, na Niyombare alikuwa balozi wa Kenya na mkuu wa ujasusi, nafasi ambayo alinyang'anywa mwaka huu.

Kama ilivyokuwa kwa Burkina Faso mapema mwaka huu, maoni ya wananchi nchini Burundi yanaonekana kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi kama namna moja ya kupinga watawala wa Kiafrika wanaotaka kutawala milele:  

Kiel kinacotokea leo Burundi ni mapaki ya kile kilichotokea mwishoni mwa mwaka jana nchini Burkina Faso, wakati mkuu wa nchi aliyetawala muda mrefu Blaise Compaore alipong'olewa madarakani na jeshi [7] baada ya kutangaza dhamira yake ya kugombea tena kipindi kingine cha utawala. Wakati hali nchini Burkina Faso bado haijatengemaa, hatua hiyo ilikuwa ya muhimu, kwa sababu wananchi waliunga mkono mapinduzi hayo, kwa sababu ya kuchoka utawala wa miongo kadhaa wa Compaore(..)lakini hali nchini Burundi ni tofauti kidogo, hususani kwa kurejea historia ya vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo iliyokwisha mwaka 2005.