Ngono, Dini na Siasa Vinapokutana Kwenye Onesho la ‘Sidiria ya Kimalaya’

Playwright Aizzah Fatima plays a character she calls a "hijabi feminist."  Credit: Courtesy Aizzah Fatima. Published with PRI's permission

Mwandishi wa michezo ya kuigiza Aizzah Fatima aliigiza uhusika anaouita “mwanaharakati haki za wanawake anayevaa hijabi.” Picha: Haki miliki ya Aizzah Fatima. Imechapishwa kwa ruhusa ya PRI

Makala haya na taarifa ya redio iliyoandikwa na Joyce Hackel kwa ajili ya kipindi cha redio kiitwacho The World kilichoonekana kwanza kwenye tovuti ya PRI.org mnamo Mei 28, 2015, na kimechapishwa hapa kama sehemu ya makubaliano ya ushirikiano wa kimaudhui.

Aizzah Fatima amekuwa akiogopa kwamba jina la igizo lake linalochezwa na mhusika mmoja, “Dirty Paki Lingerie,” (Vazi lisilofaa kuvaliwa hadharani), lingeweza kuwaudhi ndugu zake wa-Asia ya Kusini. Lakini baada ya takribani miaka mitano ya kuigiza akiwa Toronto na baadae Turkmenistan, mwigizaji huyo Mmarekani mwenye asili ya Pakistani hajali kama jina hilo linaleta karaha.

“Ilikuwa ni changamoto kubwa nilipoanza kuigiza onesho hili kupata ushirikiano wa jamii ya Waislamu wa Kimarekani,” anasema. “Mambo yamebadilika sana.”

Lengo hasa kwenye igizo hilo ni kusaili masuala ya kujitambua, ujinsia na dini kwa mtaamo wa Wamerekani sita wenye asili ya Kipakistani. Katika majuma ya hivi karibuni, Fatima na mwongozaji wake Erica Gould wamepanua kazi zao mpaka Luton, Bradford, Glasgow na London ambako wanawashirikisha Waislamu wa maeneo hayo kwenye majadiliano kupitia “mazungumzo ya mrejesho” baada ya onesho.

“Nimewahi kukutana na matukio ya baadhi ya kumbi za maonesho kuomba nikaoneshe onesho langu kwao, na baadae kuniarifu kwamba wameghairi kwa sababu ya woga,” anasema. “Kuna wakati tulikuwa Bradford, ninakodhani ni moja wapo ya miji masikini zaidi na yenye watu wengi zaidi wenye asili ya pakistani nchini Uingereza, na kulikuwa na watu kwenye hadhira yangu waliokerwa na onesho hilo. Na walisema wazi wazi, na bado alikuja.”

Neno “Paki” ni tusi nchini Uingereza, ambako lilitumika awali kwenye magazeti miaka ya 1960 kuwatambulisha Waasia Kusini, ikiwa ni pamoja na Wahindi, waafghani na Wabangladeshi.

Fatima anasema aliamua kuanza kuandika onesho hilo kujaribu kuonesha mtazamo usiozoeleka wa maisha halisi ya Wamarekani wenye asili ya Pakistani wanaoishi Marekani, na kwa sababu alikuwa ameumizwa kihisia kuambiwa kwamba hakuwa anafaa kuvaa uhusika wa waigiziji wa ki-Islamu wenye asili ya Asia Kusini.

“Kuna mtazamo wa kibinadamu kwenye uzoefu huu wa kuwa mwanamke wa Kiislamu (tena) Mmarekani aliyekuwa anakosekana kwenye vyombo vya habari, aliyekosekana kabisa miongoni mwa wahusika tunaowaona kwenye filamu, runinga, kumbi za maonesho,” anasema. “Nilitaka kumwonesha mwanamke wa Kiislamu, hususani wanawake wanaofunika nywele zao, kwa namna ninavyowafahamu, wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake na wapaza sauti wakubwa wa kushinikiza mambo.”

Fatima anasema mtazamo hasi na wa jumla kwa Waasia wa Kusini utakoma katika miongo ijayo.

“Ninatumaini kwenye maisha yangu, miaka 30 ijayo, tutaweza kutazama nyuma kuona nyakati hizi na kusema, ‘Tumevuka kipindi hicho,” anasema. “Tumepiga hatua.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.