- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Je, Saudi Arabia Imelishambulia Bwawa la Kale la Marib Nchini Yemen?

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Saudi Arabia, Yemen, Habari za Hivi Punde, Historia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Kuna taarifa zisizodhibitishwa zinazosema kwamba vikosi vya pamoja vya Kisaudi, ambavyo vimekuwa vikiishambulia Yemen kwa mabomu kwa zaidi ya miezi miwili sasa vimelilenga Bwawa la Marib [1], moja wapo ya maajabu makuu ya katika ulimwengu wa ubunifu wa kale wa kiufundi.

Kwenye mtandao wa Twita, Hussain Albukhaiti anadai:

Taarifa zisizothibitishwa: Ndege za kijeshi zimeshambulia bwawa la Mariba

Akijibu twiti hiyo, Albukhaiti anaweka picha za bwawa hilo linalokadiriwa kujengwa katika karne ya nane kabla ya Kristo na linasemekana kuwa bwawa la zamani zaidi duniani:

Uharibifu wa Bwawa la Mariba limejengwa karne ya nane (KK) na limelengwa na ndege za kijeshi za Kisaudi

Kiwango cha uharibifu wa miundo mbinu na historia ya Yemeni bado hakijajulikana. Tunaendelea kukusanya taarifa na vyanzo zaidi viko hapa [11] kuhusu tukio hilo kwenye dawati la Global Voices Uthibitisho, mradi unaowezeshwa kwa ushirikiano na Meedan Checkdesk [12], zana ya mtandaoni ya uthibitisho wa habari, pamoja na Global Voices Online.

Unaweza kuacha maoni yako hapa kuchangia dondoo kuhusu habari hii au hata kuungana na timu yetu ya habari.