Namna ya Kuwafanya Wagonjwa wa Ebola Waone Nyuso za Wahudumu Wao Nchini Liberia

Jianjay Potter and Grace Zardon in Monrovia, Liberia. Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission.

Jianjay Potter akiwa na Grace Zardon mjini Monrovia, Liberia. Picha: Marc Campos. Imechapishwa kwa ruhusa ya PRI.

Makala haya na taarifa ya habari kwa njia ya redio vimeandaliwa na  Andrea Crossan maalum kwa ajili ya kipindi cha The World awali kilionekana kwenye mtandao wa PRI.org mnamo Aprili 7, 2015, na kushapishwa tena hapa kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana maudhui.

Liberia, nchi iliyoko Afrika Magharibi imekuwa na mlipuko wa Ebola kwa mwaka mzima ambao  umeua maelfu ya watu.

Na kwa wale walio mahospitalini wakiteseka, wanachoweza kukiona ni sura za madaktari na manesi waliovalia mavazi kama roboti wakijaribu kuwahudumia. Watumishi wa afya lazima wavae mavazi haya maalum kuwakinga na maambukizi yanayoweza kutokea kwa wagonjwa wao. Lakini hali hiyo inakuwa kama inadhalilisha utu wa mwanadamu.

Mpaka sasa.

Msanii anayeishi Los Angeles Mary Beth Heffernan aliona mavazi ya kujikinga na Ebola kwenye taarifa za habari. Alifikiri namna gani mavazi ya jinsi hii yanaleta hisia za kutengwa na kubaguliwa kwa wagonjwa. Na kuanzia hapo akapa wazo la kuwapiga picha watumishi wa afya na kuziweka kwenye mavazi hayo ya kujilinda na maambukizi.

Mwishoni mwa mwezi Februari, Heffernan alisafiri kwenda Monrovia, Liberia kufanya kazi hiyo ya kupiga picha.

Alinunua kamera, mashine sita za kuchapisha, wino na karatasi maalum za kuchapishia picha.

Mary Beth Heffernan taking photograph of health worker Morris Zolu. Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission

Mary Beth Heffernan akipiga picha za mhudumu wa Morris Zolu. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

“Niliwakaribisha wahudumu wa afya kuniambia maneno ambayo wangependa kuwaambia wagonjwa wao kama wasingekuwa wamefunikwa na mavazi hayo,” anasema Heffernan. “Wengi waliamua kutabasamu nikiwapiga picha na hicho ndicho wagonjwa wao wanachokiona kwenye picha zao kubwa wanazozibadika kwenye mavazi yao.”

Health workers Morris Zolu, Kaifouba Kamara, and Joseph Walatee wearing their portraits. Credit: Marco Campos. Published with PRI's permission

Mhudumu wa afya Morris Zolu, Kaifouba Kamara, akiwa na Joseph Walatee wakiwa wamevaa picha zao. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

Picha hizo zilibandikwa kwenye mavazi hayo ya kujikinga na zilitupwa kila siku inapomalizika.

“Moja wapo ya changamoto ilikuwa ni kwamba ni vigumu kupata picha nchini Liberia na ilikuwa gharama kubwa kuzichapisha.” Kwa hiyo Heffernan aliwapa watumishi hao nakala moja ya picha zao kwa ajili ya matumizi yao binafsi.

A photo label on the back of an iPad Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission

Alama ya picha nyuma ya iPad. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

Heffernan anasema kwamba ni vizuri zaidi wahudumu wa afya kuvaa picha hizo kuliko kuvaa vitambulisho vyenye majina yao.

“Kitambulisho ni kidogo, kimejadaliwa utepe mwembamba, na kinaleta picha ya mamlaka. Kinatofautisha makundi ya watu wenye mamlaka, na kile nilichotaka ni kuwafanya wagonjwa wajisikie kuwa na mamlaka zaidi.”

Selina, a Monrovia healthcare worker, wearing her portrait. Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission

Selina, mhudumu wa afya wa Monrovia, akiwa kavaa picha yake. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

Na kwa wahudumu hao, kufanya hivyo kuliwasaidia kuhusiana vyema wao kwa wao pamoja na wagonjwa wao.

Wahudumu hao wa afya walimwambia Heffernan, “[tangu tuanze kuvaa picha zetu] hatuonekani kama watu wanaotisha.”

Health worker in Monrovia donning gloves. Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission

Wahudumu wa afya jijini Monrovia wakivaa glovu. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

Kama juhudi zitaendelea, huenda watumishi wa afya hawatahitajika kubandika picha zao kwenye nguo zao kwa muda mrefu. Mlipuko wa Ebola umekuwa ukipungua katika miezi ya karibuni na kuna matumaini kwamba nchi hiyo inaweza kutangazwa kuwa haina maambukizi ya ugonjwa huo.

Morris Zolu, Hygienist, entering Red Zone. Credit: Marc Campos. Published with PRI's permission

Morris Zolu, bwana afya, akiingia kwenye eneo lenye hatari. Picha: Marc Campos. Imetumiwa kwa ruhusa ya PRI

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.