Mchora Katuni wa Malaysia Aapa Kuendelea Kupambana na Serikali Licha ya Kushitakiwa kwa Uchochezi

From the Facebook page of Zunar Kartunis

Kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Zunar Kartunis

Mchora katuni wa Malaysia anayekabiliwa na mashtaka ya uchochezi ameapa kuendelea kutumia penseli yake kuikosoa serikali kwa ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu, na matumizi mabaya ya madaraka.

Zulkiflee Sm Anwar Ulhaque, anayefahamika zaidia kama Zunar nchini Malaysia, ni mchoraji w akatuni ambaye amewahi kuwekwa ndani mara mbli kwa mashtaka ya kuvunja sheria ya Uchochezi, iliyotungwa na wakoloni. Zunar, ambaye alikamatwa mapema mwezi huu, alishtakiwa kwa makosa tisa ya uchochezi. Akipatwa na hatia, anaweza kufungwa kwa miaka isiyozidi 43. Hivi sasa yuko nje kwa dhamana.

Zunar amekuwa mkosoaji mkubwa wa chama kinachotawala tangu miaka ya 1950. Kwa sababu ya harakati zake, vitabu vitano ya katuni zake vimepigwa marufuku nchini Malaysia. Hata wale wanachapisha, kutawanya na kuuza vitabu hivi wanapata bughudha ya serikali.

Badala ya kurudi nyuma, Zunar amegoma kutishika. Aliwahi kusema kwamba “kadri utawala unavyonoa ngumi zake za chuma, ndivyo penseli yangu inavyozidi kuwa na makali!”

Aliongeza:

Kipaji si zawadi, bali wajibu. Kw ahiyo nitakitumia kama zana ya kupaza sauti ya watu kupitia sanaa na kushinikiza mabadiliko kwa maslahi ya Malaysia. Sitanyamaza. Kwa nini nisioneshe upande, wakati hata penseli yangu huwa na upande nikiitumia?

From the Facebook page of Zunar Kartunis

Kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Zunar Kartunis

Alipoulizwa kuhusu mbinu yake, Zunar alieleza kwamba ni muhimu kwa msanii ‘kuwa na msimamo unaoeleweka‘ na kutoa ujumbe sahihi kwa hadhira yake:

Mawazo yangu hutokana na masuala yanayotokea, hususani siasa. Suala linapotokea, hatua ya kwanza ni kulielewa vizuri kwa kutumia vyanzo na mitazamo tofauti. Baada ya kukusanya taarifa zote, hatua ya pili ni kutafuta upande wa kusimamia katika suala hilo. Hatua hii ni ya muhimu kwa sababu ndiyo inayoamua mwelekeo wa katuni zangu. Msimamo sahihi unasaidia kutoa ujumbe sahhi. Sipendi kutoa ujumbe usiofaa kwa sababu tu ya kutaka kuwafanya wasomaji wacheke.

Katuni hii ilisambazwa sana baada ya Zunar kukamatwa mwezi huu. ZUnar alisema ataendelea kuchora hata kama alikuwa amekamatwa:

Katuni ya Zunar: Mpaka tone la mwisho!

Katuni hii ilitumiwa kama sababu ya mashitaka ya uchochezi dhidi ya Zunar. Najib Razak ni Waziri Mkuu aliye madarakani anayetuhumiwa na kiongozi wa upinzani anayetumikia kifungo jela Anwar Ibrahim kutumia mahakama kuwanyamazisha wakosoaji wake. Anwar, anayetumikia kifungo chake cha miaka mitano jela kwa makosa ya ufiraji, anasema kesi yake iliendeshwa kisiasa.

Katuni ya Zunar: Waziri Mkuu Najib ni hakimu!

Kikundi cha haki za binadamu Suaram kilimtetea Zunar na kuilaani serikali kwa kuwaweka kizuizini wakosoaji wake:

Kuwatesa na kuwashitaki watu kwa kutokukubaliana au kuikosoa serikali ni kinyume na misingi ya demokrasia na uwajibikaji wa serikali. Demokrasia inadai ushirikishaji huru wa raia kwenye michakato ya kisiasa, na hiyo inahusisha pia haki ya kukosoa, na haki ya kuamua [kwa sanduku la kura] serikali inayokuwa madarakani.

Zifuatazo ni baadhi ya katuni za Zunar zilizowekwa kwenye mtandao wa Twita. Zunar amekuwa mkosoaji wa kodi mpya (GST) iliyobuniwa na serikali na anaiona kuwa ni mwendelezo wa hali ya juu wa vitendo vya ufisadi. Alionesha namna kodi hiyo mpya itakavyowaathiri watu wa kawaida yaani rakyat:

Katuni ya Zunar: Asilimia 6, Asilimia 6!

Katuni ya Zunar: Raia wa kawaida asilimia 6, Serikali mfululizo wa 7

Katuni za Zunar kuhusu kupitishwa kwa sheria mpya ya uchochezi ambayo wanaharakati wanaamini itabana uhuru wa maoni mtandaoni:

Katuni ya Zunar: Sheria ya Uchochezi nchini Malaysia

Zunar alionesha sheria mpya ya kupambana na ugaidi, iliyopitishwa na bunge mwezi huu, kama hatua za kukandamiza wananchi:

Katuni ya Zunar: Sheria ya Kupambana na Ugaidi haina ubinadamu ndani yake!

Mwaka 2011, Zunar alitunukiwa “Tuzo ya Ujasiri kwenye Katuni ya Kiuchambuzi’ na Mtandao wa Kimataifa wa Haki za Wachora Katuni ulioko jijini Washngton.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.