- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuutafuta Ukristo Nchini Japani, Mahali Ambapo Imani za Kidini Hazina Umaarufu

Mada za Habari: Japan, Dini, Uandishi wa Habari za Kiraia
夕日に照らされる十字架。画像はFlickrユーザーのSharonより。 [1]

Mchweo nyuma ya msalaba. Picha na mtumiaji wa Flickr Sharon.

Kwa idadi ya waumini, Ukristo mara nyingi huonekana na dini kuu duniani. Hata hivyo, kuna Wakristo wachache sana nchini Japani, ambako chini ya asilimia moja ya idadi wa watu ni waumini wa imani ya Kikristo [2].

Nchini Japani, imani kama inavyoeleweka na kuenziwa katika nchi za Kimagharibi au kwenye utamaduni wa Kiyahudi ni nadra sana. Kwa Mjapan wa kawaida, Ukristo unahusishwa zaidi na ndoa inafungwa na kasisi kanisani [3].

Jengo zuri la kufungia ndoa(/_;)/

Kwa kutumia majina ya bandia, baadhi ya wa-Japan huingia mtandaoni kutangaza imani yao ya Kikristo. Makala moja ya blogu ilivutia maoni mengi kuhusu imani ya Ukristo nchini Japani [6].

Kwenye makala hiyo ya blogu, mwanablogu wa Kijapani asiyetumia jina lake, anaelezea kwa nini ni Mkristo:

「周囲の人はうまく出来てるのにどうして自分はできないのか」という劣等感があって、周囲の人に冷たくされる度に怒りと悔しさで泣きたくなって、なんで自分だけという気持ちだった。

よく言われるように、世界を変えるには自分が変わるしかない。

そこでひらめいてしまった。神様的なものが愛してくれると思えばもしかしていいんじゃないか?と。

こんな自分でも神様は愛してくれる、神様は認めてくれる。これが結構いい感じにはまって、気持ちは楽になるし心も落ち着いた。

正直なところ神様が居るとは思ってないし信じているとは言いがたい。

でもとりあえずそこに居るという事にして、神的なものに愛されていると思うようにしたら、それじゃあこんなに愛してくれる神的なもののために感謝しましょうと思うようになったんだけど、この感謝が非常に良い。

恥ずかしながら、今までどれだけ他人に感謝せずに生きてきたのかを思い知らされた

Mimi sijiamini na najihisi kuwa mtu duni: kwa nini watu wanaonizunguka wawe na mafanikio, wakati mimi sina kitu? Kwa hiyo wakati wengine hawanichangamkii, ninajisikia kuumia na hasira, na kushangaa kwa nini niteseke peke yangu namna hii.

Mara nyingi inasemekana kwamba kama unataka kuubadili ulimwengu, basi lazima ujibadili mweyewe. Na hilo lilinijia mawazoni. Labda ninachoweza kukifanya ni kukubali kuwa kuna aina fulani ya Mungu anayenipenda.

Nikiongea kwa ukweli kabisa, hata hivyo, siamini kwamba Mungu yupo, na ni vigumu sana kwangu kusema kwamba nina imani ya kidini.

Lakini nimejaribu kujiaminisha wakati mwingine kwamba huenda Mungu yupo na nimejichukulia kama mtu anayependwa na uwepo huo, hali inayonifanya nimshukuru kwa upendo wake mwingi kwangu. Sijawahi kujisikia vizuri zaidi ya kushukuru namna hii. Ninajisikia aibu kusema kwamba hali hiyo imenifanya nigundue namna gani siku za nyuma sikuwa mtu wa shukrani kwa wengine.

Mwanablogu huyo alijichanganya kidogo hapa; akisema anataka kuwa na imani ya Ukristo, lakini wakati huo huo akiwa hana uhakika kama Mungu yupo.

Hata hivyo, inaonekana ibada za kidini zimemfanya mwanablogu huyu kujisikia kuchanganyikiwa kwa upande mmoja pamoja na kujisikia furaha kwa upande mwingine.

ああでも待って、これって宗教にはまるコースまっしぐらじゃない?というかはまってない?

でも、一度感銘を受けたものを追い出すのは無理、もう手遅れだけど、今のところ教えは人間として生きるのに非常に真っ当な事しか言ってないので、もっと聞きたい、それに近づいて豊かな生活を送りたいという気持ちがあるんだけど、宗教だし、と思うと迷う。

親は嫌がるだろうなぁ。まああの人達は何をやっても反対するから、何をやろうとたいして変わらんか。

他人には言えないなぁ

Ah, ngoja, hii si namna ya kawaida kabisa ya kujihusisha na dini? Au tayari nina dini?

Siwezi kuachana na kitu ambacho kimegusa moyo wangu. Haiwezekani tena kufikiri upya hata hivyo. Mafundisho ya dini yananielekeza namna ya kuishi kama binadamu na kwangu hilo linafaa. Nimejiweka sawa kusikiliza, na ninaishi maisha yaliyojaa imani kwa kuendelea kuwa karibu, lakini siwezi kuamua kwa sababu dini.

Ninadhani wazazi wangu wasingenipenda niwe na dini. Na kweli, kwa sababu inanichanganya hata nifanyeje, kile ninachokifanya haleti tofauti.

Lazima nifanye hisia hizi ziwe siri.

Many commenters responded negatively [7]to the post. Mtoa maoni ajiitaye takass32 alikana uwepo wa Mungu [8].

実際には存在しない「自分に寛容且つ立派な人」を脳内にシミュレートできる、つまり信じられる事が宗教の本質なのかと思いました。

Nadhani uwezo wa kufikiri au kuamini mtu asiyekuwepo na anayeheshimiwa utafikiri yupo na kuwa na uvumilivu ndio umuhimu wa ibada za kidini.

honeybe, mtoa maoni mwingine kwenye blogu hiyo, alikuwa na maoni chanya kuhusu kuwa na imani, lakini alisaili matatizo ya dini [9].

別に宗教にハマることは悪いことではない。周りの人間に悪影響をおよぼすこと(しつこい勧誘、なにかを売りつける、宗教的観念を押し付ける等)が悪なので。

Si vibaya kuwa na dini labda kama kufanya hivyo kunaleta madhara hasi kwa watu wanaokuzunguka, kama vile kuwahubiria wengine kwa nguvu, kujaribu kueneza vipeperushi vya dini, au kuaminisha watu imani zako.

Msomaji mwingine ketudan aliona uwezekano [10] wa mwanablogu huyo kujikuta katika hatari ya kujiunga na vikundi vya dini.

残念ながらキリスト教もカルト・新興宗教だらけなので一度その教会や会派の名前でググるくらいはしておいたほうがいい。俺も昔宿題で近所の「確かな教会」に礼拝に行ったが和室でギター掻き鳴らす邪教の館だった。

Kwa bahati mbaya, kuna vikundi vingi vya dini mpya vinavyojitangaza kama “Wakristo”, kwa hiyo ninakushauri utumie mtandao wa google kupata jina la kanisa au dini ya kujiunga nayo.

Niliwahi kufanya kazi ya ziada wakati fulani kuhudhuria ibada siku za nyuma na baadae ninatembela “kanisa zuri” hapa jirani, lakini nilichokikuta ni kikanisa cha kijinga kikiwa na mtu anayejifanya mhubiri akipiga gitaa kwenye chumba chenye madhari ya ki-Japani.

gohankun alipatwa na huruma [11] kwa ugumu wa kukutana na imani za kidini nchini Japani.

日本で特定の宗教を持つというのはしんどいことだよね。クリスチャン家庭に生まれて自分もクリスチャンなので色々辛い思いもしてきたし今も時々するよ。欧米に生まれてたらどんなに楽かと何度も思ってきた。

Kwa kweli inachosha kupata dini fulani nchini Japani. Nimekutana na ugumu kwa sababu ninatoka kwenye familia ya Kikristo na mimi ni Mkristo, pia. Ninateseka wakati mwingine. Kuna nyakati ninatamani ningekuwa nimezaliwa kwenye nchi za Magharibi. Maisha yangekuwa rahisi.

Msomaji mwingine ajiitaye nows_s alihitimisha kwamba dini ni namna nyingine ya kufurahia maisha. [12]

人生は、一人で立ち向かうには重過ぎるので、神仏に帰依したり、国家にすがったり、恋愛や2次元キャラやニコチンや酒に溺れたりする。それで何とか気楽に生きてけるなら、まあ、いいじゃん

Maisha ni mafupi sana kwa mtu kuhangaika, kwa hiyo tunajikabidhi kwa miungo, kwa kweli ni kutegemea, au kulowea kwenye tabia za mapenzi, tabia mbovu, madawa ya kulevya, au pombe. Kama lolote kati ya hayo linakufanya uishi maisha ya amani, tatizo nini?