- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Jiandae kwa Mkutano wa MozFest Afrika Mashariki 2015

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Uganda, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia

MozFestEA [1] ni tukio litakalofanyika kuanzia Julai 17 – 19, 2015 kwenye Chuo Kikuu cha Victoria, Kampala, Uganda likiwa na maudhui makuu, “Kutafuta Majibu ya Changamoto za Afrika, kwa pamoja mtandaoni”:

MozFest Afrika Mashariki ni tukio la kila mwaka linalowaleta pamoja wataalam wa elmu, wabunifu, wasomi na mafundi wa Afrika Mashariki kujaribu kujadili namna ya kujenga mtandao kwa pamoja kwa kuweka msingi wa ukuaji wa mtandao wa intaneti na teknolojia ya habari barani Afrika.

Tukio hili limeenea Afrika nzima kusaidia kukabili changamoto za teknolojia zinazolikabili bara la Afrika kwa kutumia mifumo mizuri ya ushirikiano.