- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Filamu ya Malawi Yawasaidia Wakulima Kujikinga na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Malawi, Filamu, Sayansi, Uandishi wa Habari za Kiraia

Filamu ya “Mbeu Yosintha [1]” ilitengenezwa kuwasaidia wakulima na wanavijiji kujikinga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, hususani kubadilika kwa majira ya mvua kwenye ukanda wa Afrika Kusini Mashariki. Filamu hiyo ni tamthlia inayowatumia wasanii wa ndani ya nchi hiyo na iliandaliwa na mwandishi wa Kimalawi Jonathan Mbuna baada ya utafiti wa kina uliofanywa na Asasi Sizizo za Kiserikali zinazojishughulisha na kilimo nchini Malawi.