Serikali ya Masedonia Yazuia Kupiga Picha za Maandamano kwa Kutumia Kamera za Anga

Image tweeted by @Nav_urov. Photo from a drone flying above the massive December 10 student protests.

Picha twiti ya @Nav_urov. Picha ya kamera iliyokuwa ikipaa juu ya kundi la wanafunzi waliokuwa wakiandamana Desemba 10.

Jamhuri ya Masedonia imetunga kanuni mpya kuzuia matumizi ya kamera za anga kwa umbali wa mita 500 kutoka kwenye majengo ya serikali, mikusanyiko ya watu na maandamano. 

Video na picha zilizotengenezwa na kamera zinazopaa angani kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa nyenzo kubwa katika kuonesha ukubwa wa  maandamano ya wanafunzi hivi karibuni, ambayo hayakuandikwa na vyombo vikuu vya habari, lakini yakiitwa  maandamano makubwa zaidi ya wanafunzi  nchini Masedonia katika miaka 25 ya uhuru. On Desemba 10, 2014, maelfu ya wanafunzi na maprofesa wa Chuo Kikuu waliingia mtanaani kukataa mpango wa serikali wa kutoa mitihani inayosimamiwa na serikali kwa wahitimu wa chuo kikuu.

Gazeti linalounga mkono misimamo ya serikali Dnevnik daily liliandika ripoti kuhusu kanuni mpya, ambayo imekuwa ikitenda kazi tangu Januari 31, lakini ikiwa bado haichapishwa mtandaoni kwenye tovuti yoyote muhimu ya serikali.

„Не може да се вршат операции на летала без екипаж под 150 метри во секоја населено област, под 50 метри растојание од секое лице, брод, возило или инфраструктура…“, стои во уредбата.

Притоа се забранува дронот да се насочува кон лица, животни или собир на луѓе.

„Не може да лета летало без екипаж во радиус од 500 метри од објектите од значење за безбедноста, објектите на државните органи и критични народни маси, како што се објектите на Министерството за одбрана и АРМ, објектите на МВР, Владата, Собранието, резиденцијата на претседателот на државата, дипломатските претставништва, високоризични натпревари и голем собир на луѓе (протести)“, стои во уредбата.

“Hairuhusiwi kutumia kijindege cha kamera kisichoruhusiwa katika umbali wa mita 150 juu ya eneo la makazi, mita 50 kutoka kwa mtu, gari, au jengo,” kanuni hiyo inasomeka.

Kadhalika, kanuni hiyo inazuia kuelekeza kamera inayopaa kwa mtu, mnyama au mkusanyiko wa watu.

Kwa mujibu wa kanuni hiyo: “Hairuhusiwi kurusha kamera kwenye kipenyo cha mita 500 kutoka kwenye jengo linalohusika na usalama, majengo ya vyombo vya serikali na mkusanyiko muhimu wa watu, kama vile majengo ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Jamhuri ya Masedonia, majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani, serikali, Bunge, makazi ya Rais wa nchi, majengo ya Ubalozi, mashindano ya michezo yenye hatari kubwa, na mkusanyiko mkubwa wa watu (wanaoandamana).”

Mkutano wa wanafunzi, ulioandaa  maandamano ya Desemba 10 unadai kwamba mwongozaji wa kamera hiyo ya kupaa angani alikamatwa na polisi. Hakuna taarifa zilizotolewa hadharani kuhusiana na na kukamatwa kwae wala mashitaka yake.

Kijana mwenye kamera hiyo amekamatwa kwenye kituo cha Polisi cha Karposh. Shinikizo linaendelea lakini hawawezi kutuzuia. Huu ni mwanzo tu!

Miaka miwili iliyopita, makumi ya maelfu ya wa-Masedonia yaliingia mtaani kuandamana dhidi ya umasikini na ufisadi kwenye nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni mbili. Tangu wakati huo, makundi mbalimbali ya watu – wanafunzi, walimu, wakazi na wafanyakazi – wamejitokeza kuandamana, kudai mazingira bora na haki. Serikali imetumia mbinu mbalimbali kukatisha tamaa kutangazwa kwa habari za maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na kuwatisha waandishi wa habari

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.