- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Boko Haram Yaua Watu Wasiopungua 81 Huko Fotokol, Cameroon Kaskazini

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Chad, Kameruni, Naijeria, Mahusiano ya Kimataifa, Majanga, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vita na Migogoro
Northern Cameroon border, where Boko Haram operates [1]

Mpaka wa Cameroon Kaskazini, ambako where Boko Haram hufanya kazi zao

Mnamo Februari 4, Boko Haram walifanya shambulio baya [2] kwenye mji wa Fotokol Kaskazini mwa Cameroon [3], baada tu ya kuvuka mpaka wa Naijeria. Mamia wa raia wanahofiwa kupoteza maisha 81 wamethibitika kufa na Wizara ya Ulinzi [4]. Shirika la Haki za Binadamu nchini humo linaamini kwamba karibu watu 370 wameuawa [5]. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kwamba miili kadhaa ilipatikana kwenye mitaa ikiwa imechinjwa makoromeo.  Mji wa Fotokol umekuwa ukikabiliwa na vita kati ya Boko Haram na majeshi ya Cameroon na Chadi kwa siku za hivi karibuni: Machi 2014 [6], Agosti 2014 [7] na Oktoba 2014 [8]. Mwanablogu wa Cameroon Noelle Lafortune anaripoti kwamba shambulio hilo linaonesha kwamba Boko Haram inaweza kuwa inaanza kupoteza nguvu katika eneo hilo [9]:

Au front, la peur est en train de changer de camp. L'entrée en scène de l'armée tchadienne en appui aux armées camerounaise et nigériane semble être décisive, eu égard à la panique qui s'est emparée de Boko Haram.  La puissance de feu des forces coalisées a mis en déroute Shekau et sa bande. 

Kwenye mstari wa mbele, wasiwasi unakumba pande zote. Kujitokeza kwa jeshi la Chadi uunganisha nguvu na majeshi ya Camerron na Naijeria kuonekana kuwa na maamuzi sasa, imeleta hali ya tahayaruki kwa kikundi hicho cha kigaidi cha Boko Haram. Mapigano ya majeshi hayo ya pamoja yalimng'oa Shekau (kiongozi wa Boko Haram) na genge lake.