Kikundi cha raia wa Thailand kilikusanyika nje ya Ukumbi wa Sinema wa Odeon uliopo kwenye viwanja vya Leicester jijini London siku ya Jumatatu, Novemba 10, wakati wa kuonesha kwa mara ya kwanza kwa filamu maarufu ya “The Hunger Games: Mockingjay Sehemu ya 1,” kama jitihada za kufanya dunia iangazie uwepo wa hali inayotishia demokrasia, uhuru wa kujieleza, na utawala wa sheria nchini Thailand.
Filamu hiyo ina umuhimu mkubwa kwa wa-Thai wengi. Kwa hakika, wapinzani wa mapinduzi ya kijeshi hivi majuzi nchini Thailand, yaliyoiong'oa madarakani serikali iliyokuwa imechaguliwa kidemokrasia iliyokuwa ikiongozwa na Yingluck Shinawatra, na waliweza kuiga alama ya vidole maarufu ya vitatu inayoonekana kwenye filamu hiyo. Alama hiyo imekuwa maarufu sana kiasi kwamba jeshi la nchi hiyo limeipiga marufuku, ikiwa ni pamoja na upinzani mwingineo wa kisiasa. Mamia ya wa-Thai hivi karibuni yalitumia salamu hiyo kwenye mazishi ya Naibu spika wa zamani Apiwan Wiriyachai, kwa kumsalimia Yingluck Shinawatra kwa ishara hiyo, alipowasili kutoa heshima zake za mwisho.
Katika kusanyiko hilo juma hili jijini London, wengi wa wanaharakati hao walilazimika kuvaa magamba ya kuficha nyuso zao, kwa hofu ya kuwasababishia matatizo ndugu na jamaa zao walioko nchini Thailand.
Wanaharakati hao walifungua ukurasa wa Facebook na akaunti ya Twita katika kuratibu jitihada zao, kwa kutumia alama ishara #DistrictThai. “District” inaaminisha mkakati ulioitwa “The Hunger Games,” ambapo udikteta wa kiimla unaoanzia mahali fulani hutawala maeneo mengine ya kijiografia yanayoitwa wilaya (“districts”). Maeneo haya yamefukarishwa na kutumikishwa na “Makao Makuu.”
Anuani hizo za mitandao ya kijamii zinaendeshwa kwa lugha za ki-Thai na Kiingereza, kwa ajili ya hadhira ya nyumbani huko Thailand na duniani kote. Ukurasa wa Facebook wa kundi hilo ulikuwa maarufu, ukivutia watu 1,000 kuupenda ndani ya mwisho wa juma moja pekee. Ujumbe wa kwanza ulionekana Ijumaa, Novemba 7:
Wafanyakazi wa Ukumbi wa Sinema wa Odeon jijini London, walipogundua maandamano ya #DistrictThai, waka twiti:
#DistrictThai are in town and they look awesome. A for effort! #mockingjay pic.twitter.com/DlSlDokSgO
— ODEON (@ODEONCinemas) November 10, 2014
Maandamano ya #DistrictThai yako jijini na yanaonekana poa. Nawapa alama A kwa jitihada zao!
1 maoni