- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Video: Mwanasheria wa Swaziland Aliyefungwa Jela Azungumza Kupitia Wanaharakati wa Haki za Binadamu

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Swaziland, Haki za Binadamu, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

#swazijustice [1] ni kampeni inayotoa wito wa kuachiliwa huru kwa Bheki Makhubu, mhariri wa gazeti la Taifa na Thulani Maseko, mwanasheria wa haki za binadamu, ambao walifungwa jela nchini Swaziland kwa miaka miwili kwa sababu ya kuandika makala kukosoa mfumo wa mahakama nchini humo. Wawili hao walikamatwa tarehe 17 Machi 2014 na kuhukumiwa kifungo cha jela cha miaka miwili mnamo Julai 25, 2014.

Kampeni ya video ifuatayo inamwonesha Rais wa RFK Center [2] Kerry Kennedy, Askofu Mkuu Desmond Tutu [3] na wanaharakati wengine wa haki za binadamu wakisoma taarifa iliyoandikwa na Thulani Maseko akiwatetea watu wa Swaziland: