- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuelimisha Wasichana Leo, Kuwawezesha Wanawake Kesho

Mada za Habari: Amerika Kusini, Venezuela, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Marita Seara [1], anayeblogu kwenye Voces Visibles [2] (Sauti Zinazoonekana), anatukaribisha kutafakari suala la ubaguzi unaowaathiri wasichana na vijana wanaopevuka —kupata elimu– na hitaji ya kuwaelimisha wasichana wetu leo ili waweze kuwa wanawake waliowezeshwa kesho na keshokutwa.

FotografÍa extraída del blog Voces Visibles, utilizada con autorización.

Picha kutoka blogu ya Voces Visibles, imetumiwa kwa ruhusa.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kutetea haki za binadamu duniani Amenisty International [3], wasichana milioni 41 hawana fursa ya kupata elimu ya msingi. Ujinga, ndoa za umri mdogo, mimba za utotoni ni sehemu ya mduara usiokwisha [4] unaoathiri maisha ya wasichana. Kwa hali hiyo, Amerika ya Kusini haikwepi suala hilo la kidunia, kuhusu mimba za utotoni:

Venezuela ostenta el primer lugar en Suramérica y el tercer lugar en América Latina al ser el país con mayor cantidad de embarazos precoces. De cada 100 mujeres venezolanas que quedan embarazadas anualmente, 25 son adolescentes, de acuerdo al programa de Telemedicina de la Universidad Central de Venezuela.

Venezuela inaongoza orodha ya nchi za Amerika Kusini na ni ya tatu kwenye eneo la Amerika ya Kati ikiwa na kiwango kikubwa kabisa cha mimba za utotoni. Katika wanawake 100 wa Venezuela wanaopata ujauzito kila mwaka, 25 ni watoto wanaopevuka, kwa mujibu wa mpango wa Telemedicine unaoendeshwa na Chuo Kkuu cha Central Venezuela.

Kati ya sababu za mimba za utotoni, theluthi moja ya mimba zisizotarajiwa ni matokeo ya utokutumia kinga, na nuu ya wasichana wanaoathirika ni wale ambao hawakupata elimu ya afya ya uzazi kabla ya kupata mimba.

Kwa hiyo, elimu ni njia moja pekee. Kwa kuwaelimisha wasichana wetu leo, tunawawezesha wanawake wa kesho, na hivo, familia na jamii zao.

Unaweza kumfuatilia Marita Seara kwenye Mtandao wa Twita [5].

Posti hii ni sehemu ya ishirini na saba ya #LunesDeBlogsGV [6] (Jumatatu ya blogu kwenye GV) mnamo Novemba 3, 2014.