Waandishi wa Hong Kong Wapambana na Udhibiti wa Habari Unaofanywa na Vyombo vya Habari

Staffs from Apple Daily News showed their determination to keep the news room operating after the mob attack on October 13. Photo from Chan Pui Man's Facebook.

Wafanyakazi wa Jarida la kila siku la Apple Daily wakionesha msimamo wao wa kuendelea kufanya kazi hata baada ya kushambuliwa mnamo Oktoba 13. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Chan Pui Man.

Waandishi wanaofanya kazi nchini Hong Kong wamejikuta kwenye shinikizo kubwa katika majuma mawili yaliyopita kwa uamuzi wao wa kuandika habari zinazohusu Mapinduzi ya Mwamvuli, maandamano yanayodai demokrasia kupitia uchaguzi ulio huru na haki. Si tu kwamba wamejihatarisha kwa ghasia wakati wakiandika habari hizo za mapambano kati ya polisi na waandamanaji, lakini pia waliporudi ofisini wakitokea kwenye uwanja wa habari, wengine wao wamejikuta wakifuatiliwa ndani kwa ndani na waandishi wenzao au hata kujikuta wakibughudhiwa na wahuni wanaounga mkono msimamo wa Beijing.

Tangu polisi waanze kuondoa vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji kwenye maeneo yaliyopewa jina la Maandamano ya Kukaa Katikati ya Mji, mapigano kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi yametokea kila siku. Wakisimama kati ya polisi na waandamanaji, wapiga picha wa vyombo vya habari nao wamejikuta katika mazingira ya kujihatarisha. Si jambo la ajabu sasa kuona wapiga picha wa televisheni wakinyunyuziwa maji ya kuwasha au kusukumwa na maafisa wa polisi wakati wakitekeleza shughuli zao. Katika matukio mengine, polisi hawawatofautishi waandamanaji na wanahabari na hivyo kuwabughudhi wakati waandishi hao wakipiga picha za waandamanaji walio msitari wa mbele.

Tovuti nne huru mpya — inmediahk.net, SocREC, USP na Local Press — zilitoa tamko la pamoja kuwalaani polisi kwa kuwavamia waandishi kwa makusudi kabisa siku ya Oktoba 15 walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji kwenye barabara ya Lung Wo iliyoko nje ya makao makuu ya serikali:

凌晨三點,SocREC一名攝影記者則在添馬公園採訪清場,被持防暴裝備的警察強行拉入警員堆之中,拳打腳踢接近30秒,記者的眼鏡、頭盔以及眼罩被打至飛脫。一輪暴打後,兩名警員把該名記者拖行近30秒,送上警察押送犯人的旅遊巴上。拖行期間,受傷記者不停向警察展示記者證,但警察依然没有停止毆打,更用粗口辱罵記者。記者在旅遊巴上,有負責應付傳媒的警員確認SocREC記者身份後,著令他下車。記者事後已去瑪麗醫院驗傷,證實面部、額頭、鼻、嘴角、頸部以及左手手臂都有明顯傷痕。

同一時間,獨媒其一中名攝影記者在龍和道隧道內採訪期間,一名警察突然上前用胡椒噴霧指嚇他,記者遵從警員指示後退,但警察仍然在毫無警示下多次正面對準記者面部發射胡椒噴霧;後來,該記者雖然多次重申記者身份,警察仍然把他雙手扭轉並押走。其後警察更對記者吆喝:「記者又點,記者大哂?」、「記者又點,記者唔可以行前影相架嘛!」,警察確認記者身份之後放行。而另一名獨媒記者在後退時,亦遭警員用圓盾撞傷頭部。

Saa 9 alfajiri, wakati akiandika habari za kutawanywa kwa watu kwa nguvu kwenye Bustani ya Tamar, mwandishi wa SocREC alivutwa kuelekea walikokuwa polisi na alipigwa kwa sekunde 30. Baadae, maafisa wawili wa polisi walimburuta barabarani kwa sekunde 30 na kumtupia kwenye gari la polisi. Mwandishi huyo aliyepatwa na mkasa huo wakati wote alikuwa akionesha kitambulisho kilichokuwa kikionesha kwamba yeye ni mwandishi, lakini hilo hata halikuwasumbua polisi kuacha vitendo hivyo. Badala yake, waliendelea kumtukana. Baade aliruhusiwa kuondoka baada ya polisi anayehusika na habari kukithibitisha kitambulisho chake. Mwandishi huyo alitafuta matibabu kwenye hospitali ya Queen Mary na taarifa ya matibabu yake inathibitisha kuwa amepata majeraha kwenye uso wake, utosi, pua, mdomo, shingoni na kwenye mkono wa kushoto.

Vivyo hivyo, mwandishi wa mtandao wa inmediahk.net aliyekuwa akiandika habari akiwa kwenye kinjia pembeni mwa Barabara ya Lung Wo Road alitishwa na polisi na bomba la maji ya kuwasha. Alifuata masharti ya polisi na akaacha kufanya kazi yake, lakini hata hivyo bado alimwagiwa maji ya kuwasha usoni bila kupewa onyo; ingawa alionesha kitambulisho chake wakati wote, bado alikamatwa na kupigwa pingu. Wakati mwandisi huyo akionesha kitambulisho, polisi alikuwa akipiga kelele: “Mwandishi? Sasa mimi nifanyeje kwa kujua hivyo?“ “Hata waandishi hawaruhusiwi kupiga picha kwenye uwanja wa mapambano.” Mwandishi huyo aliachiwa baada ya kitambulisho chake kuthibitishwa. Mwandishi mwingine wa mtandao wa inmediahk.net alipigwa kichwani na afisa wa polisi kwa kutumia ngao ya polisi wakati akiondoka eneo hilo.

Ingawa waandishi wanaokuwa uwanja wa mapambano huhatarisha maisha yao kwa minajili ya kuandika habari, bado habari zao wakati mwingine haziandikwi kwa sababu ya kufuatiliwa kunakofanywa ndani ya vyombo vya habari. Mashirika mengi ya habari jijini Hong Kong, jimbo maalumu ya kiutawala la China, yamekuwa na hofu ya kupoteza mapato ya matangazo ya ki-Biashara kutoka bara China au kuogopa kuikasirisha serikali ya Beijing. Hali hii imeongezeka kadri maandamano hayo yanavyozidi kutoa wito wa mfumo wazi wa uteuzi wa mgombea wa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa jiji hilo, dai ambalo linapingana na matakwa ya bara ya kuwa na kamati inayohodhiwa na watu wenye mrengo wa Beijing. 

Mnamo Oktoba 15, mkuu wa matangazo wa TVB, kituo kikuu maarufu cha matangazo cha jiji hilo, kiliamuru timu yake ya habari kuhariri sauti iliyokuwa ikielezea taarifa ya video inayodaiwa kuwa ya ukatili wa polisi. Kipande hicho kinaonesha bayana mwanandamanaji aliyefungwa pingu akipigwa mateke na mafisa kadhaa wa Polisi kwenye kona iliyokuwa gizani kwa dakika nne.

Siku iliyofuata, watumishi 28 wa chumba cha habari walitoa tamko la pamoja wakionesha kusikitishwa na uamuzi huo wa utawala wa chombo hicho cha habari. Hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 100 wa kituo hicho wametia saini tamko hilo.

Mwandishi wa zamani wa TVB Au Ka Lun alieleza namna chumba cha habari cha TVB kinavyofanya kazi baada ya kusoma tamko hilo la pamoja:

這份行文平淡的聲明,一字一句,都是血與淚;我讀到了,我記起了,我們這一代記者,無止境的屈辱與掙扎,理想與現實的差距,去與留之間的徘徊。[…]
很多時,前綫記者,就只負責採訪,他們是「車衣女工」,只是新聞製作過程的一環。很多時,採訪完畢,片段送回公司,稿不是他們寫的,內容的編輯與選材,也不是前綫記者全權決定的,新聞部裡,有很多編輯,有很多採主,編輯採主之上,還有一個人;一個人之上,有強橫的勢力。記者最自由自主的時間,就是那一個人睡覺的時間,而他睡很少。

Kila neno tamko hili la wazi limeandikwa na damu na jasho. Nimelisoma na kukumbuka unyanyasaji usiokoma na mapambano ambayo kizazi chetu cha waandishi wa habari kimekabiliana nayo. Pengo kubwa kati ya hali halisi na ile iliyotarajiwa na ikiwa mtu anapaswa kuondoka au kubaki ni sula la mapambano. […]
Muda mwingi, waandishi waliokuwa mstari wa mbele ndio wanaowajibika kwa mahojiano na kurekodi kile kinachotokea kwenye eneo la tukio. Wanakuwa kama wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye duka la jasho, wanaowajibika katika shughuli ya kuandika habari. Baada ya kufanya kazi yao, video zao hutumwa kwenye vyumba vya habari. Na huwa hawawajibiki na walichokituma. Maudhui na lengo la habari huwa haliwezi kuandaliwa na waandishi. Kwenye vyumba vya habari, kuna wahariri wengi wa habari na majukumu na juu yao kuna mtu mwingine mwenye sauti ya mwisho. Juu ya mtu huyo kuna shinikizo zaidi. Waandishi hawana uhuru na hawajitegemei; wanakuwa huru wakati tu huyo jamaa mwenye sauti ya juu amelala, lakini hilo huwa ni nadra kutokea.

‘Shinikizo kubwa’ linalorejelewa hapa na Au ni mashinikizo ya aina mbalimbali ya kisiasa kutoka Beijing, kama vile vitisho. Vyombo vya habari jijini Hong Kong vimelegeza msimamo wao kwa kuwa utaratibu wa kufuatiliana weyewe ndani kwa ndani kamainavyofanyika kwenye kituo cha TVB. Kwa wale wanaogoma kulegeza msimamo, wanatishwa.

Tangu Oktoba 12, wahuni wanaounga mkono msimamo wa Beijing walipangwa kuzunguka makao makuu ya gazeti linaounga mkono demokrasia na kuwazuia wafanyakazi wa gazeti hilo kutawanya magazeti. Wahuni hao walifunga lango kuu la kuingilia kwenye jengo la gazeti hilo mnamo tarehe 13 Oktoba na kuzuia magazeti kupandishwa kwenye magari ya kusambaza. Kama vile haitoshi, tovuti ya gazeti hilo imevamiwa na kuipoteza hewani na laini za simu zilifurikwa na simu za matusi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.