Pamoja na Tishio la Ebola, Waafrika Magharibi Waendelea Kutulia na Kuikumbusha Dunia Wao Ni Nani

Screen capture from "Ebola: A Poem For The Living," YouTube.

Picha mnato ya video ya “Ebola: Utenzi Kwa Wanaoishi,” kwenye mtandao wa YouTube.

Wakati idadi iliyothibitishwa ya  vifo vilivyotokana na Ebola  inakaribia 5,000, huku kukiwa na matukio ya wagonjwa wasiopungua 10000, wananchi wengi katika eneo la Afrika Magharibi wanatumia nguvu ya mitandao ya kijamii katika kupambana na virusi vya ugonjwa huo.

Mmoja wapo wa miradi ya namna hiyo ni Ebola Alert nchini Naijeria:

EbolaAlert ni kundi la wataalamu wanaojitolea kufanya kazi kwa kutumia ushahidi katika mapambano dhidi ya virusi vya Ebola.

Lilianzishwa na madaktari lakini linajumuisha wataalam wengine wenye shughuli mbalimbali.

Mradi huo unatumia mtandao wa Twita kuposti habari zinazohusiana na Ebola kila siku na kuratibu majadiliano yanayohusu virusi vya Eloba kati ya wataalam na umma wa wananchi. Unaweza kupata taarifa muhimu kwa kuwafuatilia tunayoyafanya kwenye mtandao wa Twita

Masuala yanayohusu maabukizi ya virusi hivyo huajadiliwa kwenye alama habari ya #EbolaNews ambayo huchapishwa kati ya saa 1 na 2 asubuhi kwa saa za Afrika Magharibi kadhalika kupitia alama habari ya #EbolaScience ambapo masuala yanayochanganya ya Ebola hushughulikiwa na kujadiliwa kwa kina.

Majadiliano yanayofanyika kwenye #EbolaChat huwa ni matukio ya kwenye mtandao wa Twita ambapo wataalamu kutoka duniani kote huwepo kujadili mada zinazokuwa zimechaguliwa na watu wenyewe. Kumekuwa na majadiliano ya #EbolaChat kuhusu masuala mengi kuliko unavyoweza kufikiri

Nchini Sierra Leone, Hannah Foullah anatumia mtandao wa facebook kupambana na unyanyapaa dhidi watu wenye Ebola. Anaongoza kampeni inayoitwa “Urembo kwa Nchi yangu: Mimi ni m-Sierra Leone kwa asilimia 100, si Kirusi” akishirikiana na wenzake kama Elvinah Ade Johnson ana Haja Mariatu Thomas.

Katika video iliyowekwa kwenye chaneli ya BBC kwenye mtandao wa YouTUbe, Foullah anasema kampeni hiyo inatarajiwa kuimarisha utambulisho wa nchi ya Sierra Leone.

Hapa chini unaweza kuona picha zilizowekwa kwenye ukurasa wa facebook wa kampeni hiyo ya “Urembo kwa Nchi yangu”:

Beauty for Country photo posted on  Hannah Foullah Facebook page.

Picha ya Urembo kwa ajili ya nchi yangu iliyochapwa na Hannah Foullah kwenye mtandao wa Facebook.

ebola2

ebola3

ebola4

Nchini Marekani, shirika lenye makazi yake jimboni Nashville linaloitwa  United Methodist Communications[Mawasiliano ya Pamoja ya Kimethodisti] limeshirikiana na  Chocolate Moose Media na iHeed kutengeneza video ya vikaragosi , “Ebola: Utenzi kwa Wanaoishi,” itumike Afrika Magharibi kusaidia kuondoa imani potofu kuhusu maambukizi ya virusi vya Ebola. Video hiyo pia inaelimisha kuenea kwa ugonjwa. Kundi hilo linapanga kuitafasiri katuni hiyo katika lugha zingine kadhaa za Afrika Magharibi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.