Siku ya Blogu Oktoba 16: Shiriki Mjadala wa #KutokuwepoUsawa katika Jamii

Looking out across the bay at some of the most expensive land in the world. Image by Shreyans Bhansali (CC BY-NC-SA 2.0) https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/2.0/ Image by Shreyans Bhansali (CC BY-NC-SA 2.0)

Kutoka ng’ambo ya ufukwe wa Chowpatty, Mumbai kutazama eneo moja wapo ghali zaidi duniani. Picha na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Shreyans Bhansali mnamo Januari 9, 2007. (CC BY-NC-SA 2.0)

Tumia fursa ya kuiambia dunia mtazamo wako kuhusu dhana ya kutokuwepo usawa. Andika simulizi lako, sambaza kwa watu mtazamo huo, jadili na jenga hoja. Fanya hivyo Alhamisi hii, Oktoba 16 kwenye Siku ya Wajibu wa Blogu Duniani kwa kushirikiana na maelfu ya wanablogu wengine.

Blog Action Day 2014

Wanablogu, tuungane!
Tangu 2007, Siku ya Wajibu wa Blogu imekuwa ikitumika kuwaweka pamoja wanablogu kutoka duniani kote ili kujadili mada muhimu zinazokuwa zimewekwa mezani. Kwa pamoja, huwa utaratibu wa kuvamia anga la blogu kwa kuchapisha maelfu ya posti kuhusu masuala ya maji, mabadiliko ya tabia nchi, umasikini, chakula na nguvu ya pamoja. Ni mradi mzuri unaojenga mazoea ya wajibu wa pamoja duniani, familia kidunia, na kuibua mjadala mkubwa. Kwa hiyo kwa mara nyingine mwaka huu, Global Voices Online inayo fahari kuwa mshirika rasmi wa siku hiyo.

Nikisema kutokuwepo usawa, wewe unasema…?
Neno kutokuwepo usawa linaweza kufananishwa na mengi. Mengi sana; jambo ambalo ndilo hasa sababu ya kuifanya mada hii kugonga vichwa vya habari kwenye maeneo mengi. Kutokuwepo kwa usawa kunaweza kumaanisha kutokuwepo kwa usawa kwenye huduma za afya, ubaguzi wa rangi, jinsia, masuala ya kijamii, na dhana nyinginezo. Toa maoni yako na uzoefu wako kwenye blogu yako, na tusimame pamoja kujadili kila aina ya hali za kutokuwepo kwa usawa.

Ungana na #WajibuwaBlogu14
Kushiriki kwenye Siku ya Wajibu wa Blogu, unaweza kuandikisha blogu yako kwenye Tovuti maalum ya Siku ya Wajibu wa Blogu  – na bainisha kwamba unaweza kuandika makala yako katika lugha yoyote, kutoka nchi yoyote. Wakati wa kuandikwa kwa makala haya, washiriki 1032 kutoka nchi 108 wamejiandikisha kushiriki. Kwenye mtandao wa Twita, fuatilia alama habari zifuatazo #Blogaction14, #Inequality, #Oct16

Mnamo Oktoba 16, tutaorodhesha makala kutoka kwa waandishi wa Global Voices duniani kote – kaa mkao wa kula!

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.