Salamu ya ‘vidole vitatu’ Yaleta Matumaini kwa Wanaharakati wa Demokrasia Nchini Thailand

Katika picha inayofanana na filamu za Hollywood, watu waliohudhuria zoezi la uchomaji wa mwili wa aliyekuwa naibu spika wa Thailand Apiwan Wiriyachai walionesha ishara ya vidole vitatu kumsalimia Waziri Mkuu wa nchi hiyo Yingluck Shinawatra, katika kile kinachoonekana kuwa ni ujumbe mpya wa matumaini kwa nchi ya Thailand.

Tafadhali fahamu: bado wapo wananchi wengi wanaopinga mapinduzi ya kijeshi wanaokataa kunyanyaswa na jeshi

Picha hiyo, iliyochapishwa awali kwenye  ukurasa wa facebook wa BBC Thailand  imesambazwa kwenye mtandao huo mara 650 na kwenye mtandao wa Twita mara 70, ikiwa ni pamoja na kuchapiswa kwa mara nyingine (re-tweet) na wananchi wa Thailand wenye wafuasi wengi kwenye mtandao wa Twita  @toyubomm. BBC iliweka ukurasa huu wa Facebook kama jitihada zake za kukwepa mashambulizi kuhusu masuala ya utawala wa sheria na dhana ya uhuru kufuatia mapinduzi ya mwezi Mei, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kwa mikusanyiko ya kisiasa na kukamatwa kwa mamia ya wanasiasa na wanaharakati wanaopinga mapinduzi ya kijeshi.

Ishara hiyo ya heshima kwa kunyanyua mikono, iliyohamasishwa na tangazo la biashara la “The Hunger Games,” imekuwa ikichukuliwa kama alama isiyorasmi ya waaharakati wasiokubaliana na mapinduzi ya kijeshi pamoja na watu wanaounga mkono harakati za kidemokrasia.

Hayo yanatokea kwenye mtandao wa Facebook na Twita katika wakati ambao kuna tahayaruki kubwa nchini humo, kufuatia kitendo cha jeshi kuendelea kugandamiza uhuru wa maoni mtandaoni katika nchi hiyo. Baada ya kuwa wamechukua hatua za kuwafuatilia wananchi kwenye mitandao ya kijamii na kufungia mamia ya tovuti zinazodhalilisha wengine, ikiwa ni pamoja na  tovuti ya Daily Mail , wiki iliyopita blogu maarufu za kisiasa nchini Thailand kwenye tovuti ya Asian Correspondent, Bangkok Pundit, ilitangaza kwamba itasitisha kazi zake ikiwa ni matokeo ya “kubanwa kwa mazinira ya kutoa maoni waziwazi kuhusiana na siasa za Thailand tangu mapinduzi yafanyike.”

Wakati kufungwa kwa blogu hiyo isiyofahamika mmiliki wake ni kurudishwa nyuma kwa uhuru wa kujieleza kw watu wa Thailand, kusambaa kwa picha za heshima ya vidole vitatu mtandaoni kunaleta matumaini mapya ya mstakabali wa nchi hii iliwahi kuwa wazi na ya kidemokrasia. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.