Raia wa Guinea Waendelea Kuwa Wavumilivu Pamoja na Uwepo wa Ebola

 

Young girl in  Conakry, by Sebastián Losada - Creative Commons Attribution-Share Alike 2.0 Generic

Msichana mmoja akiwa jijini Conakry, na Sebastián Losada – Creative Commons Attribution-Share Alike 2.0 Generic

Mlipuko wa Ebola unazidi kuenea kwa kasi kiasi cha kuibua hofu kuu duniani kote. Watu  wa Afrika ya Magharibi, ukanda ambao gonjwa hili la mlipuko lilianzia, wako chini ya uangalizi mkali wa wataalamu wa afya wa kimataifa. Guinea, ambayo tayari ilishakabiliwa na tatizo kubwa la kiuchumi miongoni mwa raia wake kabla ya kulipuka kwa ugonjwa huu,  hadi sasa imeshaathiriwa vibaya na gonjwa hili. has suffered the brunt of the epidemic. Hata hivyo, raia wa Guinea wanaridhika na hali halisi ya changamoto za kimaisha zinazowakabili, hatari zilizopo, majonzi ikiwa ni pamoja na mataifa mengine duniani kuingalia Guinea kwa tahadhari kubwa.

Wanablogu wawili kama walivyonukuliwa wanafafanua namna raia wa Guinea walivyo na utayari wa kukabiliana na maisha.

Alimou Sow, ni mwanablogu wa Guinea, aliyeamua kula Pizza akiwa na mke wake pamoja na baadhi ya marafiki zake katika mgahawa mdogo ulioko pembezoni mwa Conakry, mji mkuu wa Guinea. Aelezea uhalisia wa maisha ya kila siku katika jiji la Konakry akiwa na hali ya uchangamfu usio na mashaka:

Vu de l’intérieur, le pays est comme ostracisé. Le vrombissement des avions dans le ciel de Conakry a considérablement diminué. Les étrangers ont fait leurs bagages, désertant les zones minières, les hôtels, les restos et … la bande passante sur Internet ! Depuis quelque temps, la connexion est devenue étonnamment fluide. Les téléchargements sont lénifiants. Vu de l’extérieur, sous le prisme des médias – nouveaux et anciens – toute la Guinée n’est qu’un océan d’Ebola. Beaucoup se sont barricadés de peur d’être contaminés. L’amitié, la solidarité et la convivialité ont laissé place à la suspicion et à la stigmatisation. Ebola va certainement faire son entrée dans les cursus de formation en relations internationales. L’épidémie a ouvert un nouveau chapitre pour cette discipline. Pourtant, nous vivons. Le cœur de Conakry palpite. Toujours le même chaos sur les deux principaux axes routiers : les mêmes taxis jaunes indélicats, les mêmes cadavres de Magbana chargés à ras bord, le même joli vacarme qui rythme la vie des habitants de ma capitale avec les klaxons qu’on pousse à fond, les invectives, les aboiements desCoxeurs qui arrondissent leur fin de journée par de petits larcins sur les passagers. Les marchés sont bondés, les cafés animés. Les rumeurs et les ragots, l’essence même des Conakrykas, vont bon train.

Kwa mtazamo yakinifu, ni kama vile nchi yetu imeshatengwa na jamii ya kimataifa. Kelele za eropleni zilizokuwa zikisikika kutoka katika anga la jiji la Conakry zimepungua kwa kiasi kikubwa kabisa. Wageni wameshakusanya vilivyo vyao, wameyakimbia maeneo ya uchimbaji madini, hoteli na migahawa… na pia kasi ya intaneti imeongezeka. Kwa kipindi fulani sasa, mtandao wa intaneti umekuwa unapatikana kwa urahisi na wa kasi nzuri. Upakuaji kutoka mtandaoni umekuwa unaridhisha sana. wakati huo huo, jamii ya kimataifa, kupitia upashanaji habari za kisasa na wa zamani, inaitazama Guinea kama vile haikuwa chochote bali ni chanzo kikuu cha ugonjwa wa Ebola. Wengi wamejifungia majumbani kwao wakihofia kuambukizwa ugonjwa huu. Hali ya urafiki, umoja na mshikamano imegeuka na kuwa hali za kutiliana mashaka na kukwepana. Kwa hakika, ugojwa wa Ebola utalazimisha kuwepo kwa masomo ya muda mfupi kuhusiana na masuala ya uhusiano wa Kimataifa. Ni dhahiri kuwa, gojwa hili la kuambukiza limeshafungua ukurasa mpya kuhusiana na masuala haya ya uhusiano wa kimataifa. Bado tunaishi. Maisha ya raia wa Conakry bado yanaendelea. Kero ni ileile katika barabara kuu mbili: ukatili ni uleule kutoka kwa wamiliki wa teksi za njano , hali ni ile ile ya miili ya binadamu kukusanywa kama samaki kwenye magbana mabasi kama teksi, sauti zilezile ziongezazo furaha ya maisha katika jiji langu. Sauti ya baragumu inayoongezeka kwa kasi, matamko ya kulaani pamoja na kelele za vibaraka wanaonadi, ambao humaliza siku yao kwa wizi wa wazi wanaofanyiwa abiria. Watu wamejazana masokoni, Pilikapilika katika migahawa imepamba moto. Fununu na majungu, ambayo ni mambo muhimu jijini Conakry, yanazidi kumea kwa kasi.

Cireass, mwanablogu mwingine anayeandika kuihusu Guinea, alichagua njia isiyo ya mkato katika kulielezea gojwa la Ebola pamoja na changamoto za kuielimisha jamii:

S’il y a une grande erreur que certains de nos compatriotes – ce n’est pas propre qu’aux Guinéens – ont commise dans la lutte contre la fièvre rouge, c’est bien d’avoir politisé une situation qui n’a rien de politique. Dès l’annonce de la présence de l’épidémie, ils ont nié catégoriquement son existence, sans chercher à comprendre quoique ce soit. Résultat : les installations de MSF à Macenta ont été saccagées par des gens qui criaient au mensonge [..] personne n’a intérêt à inventer une telle histoire. Ni les autorités guinéennes, ni les ONG et les organisations internationales ne pourraient tirer profit en inventant une épidémie effrayante comme celle-ci. Nous ne devons pas voir la politique derrière tout ce que nous entendons. Aujourd’hui à cause d’Ebola, la Guinée est complètement isolée sur le plan international. la meilleure façon pour nous de sortir de cette lamentable situation, c’est de combattre Ebola (ensemble), notre véritable ennemi.

Pamoja na kuwa siyo raia wa Guinea tu ndio waliokwisha fanya hivi, kosa moja kubwa wanalolifanya viongozi wetu katika vita dhidi ya homa ya dengue ilikuwa ni kuingiza siasa katika jambo ambalo halikuhitaji siasa. Tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu, watu hawakuamini kuwepo kwake na bila hata ya kutaka kujua undani wa ugonjwa huu. Matokeo yake: Madaktari Wasio na Mipaka katika jiji la Macenta walipotoshwa na watu walionadi kuwa, ugonjwa huu ulizushiwa tu kuwepo[…], pamoja na kuwa hakuna mtu ambaye angaliweza kufaidika kwa kutunga na kuzusha kupepo kwa ugonjwa wa ebola. Siyo tu kwa serikali ya Guinea wala mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa yangeweza kufaidika kwa kutengeneza aina hii ya gonjwa linalotisha. Hatupaswi kuhusisha kila kitu na ushawishi unaochochewa na siasa. Na sasa, kwa suala la ebola, Guinea imebaguliwa kabisa katika jukwaa la kimataifa. Namna pekee ya kukabiliana na bahati mbaya hii ni kufanya kazi kwa pamoja, kukabiliana na ebola, ambao ndio adui yetu wa kweli.

Ni muhimu pia kuwa na angalizo kuwa, katika harakati za kukabiliana na ebola, baadhi ya maeneo ya metropolitani kama vile ya jiji la Télimélé, yamekuwa na kinga kubwa ya kukabiliana na kirusi cha ebola kuliko maeneo mengine, ishara ya matumaini inayoweza kudhibitisha umuhimu wa tafiti za kitabibu zinazoendelea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.