Habari kutoka Oktoba, 2014
Wenyeji wa Visiwa vya Pasifiki Waizuia Meli za Makaa ya Mawe Kupinga Mabadiliko ya TabiaNchi
Kwa kutumia ngalawa zilizotengenezwa kwa mkono, washujaa wa mabadiliko ya tabianchi, wakishirikiana na raia wa Australia, waliweza kuzuia meli 10 zilizokuwa zitumie bandari ya Makaa ya mawe ya Newcastle.
GV Face: Mazungumzo na Mwanaharakati wa Bahrain Ambaye Bahrain Isingependa Tumsikie

Bahrain imeingia mwaka wa tatu ya mapambano na wanaharakati. Taarifa za vyombo vya habari vya Kimataifa zinadai maandamano hayo ni mapinduzi yanayoongozwa na Shia dhidi ya utawala wa Sunni, lakini wanaharakati wanasema hayo ni maelezo mepesi.
Hukumu ya Haki? Ina uzito wa Kutosha? Oscar Pistorius Amehukumiwa Kifungo cha Miaka Mitano Jela
Mkimbiaji wa Afrika Kusini aliyepatwa na hatia kwa kumwuua pasipo kukusudia rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp imelinganishwa na hukumu ya jangili aliyefungwa miaka 77 jela kwa kumwuua faru mwezi Julai
Uandishi wa Habari Unapokuwa Haitoshelezi

Andiko la mada ambayo inahitaji majibu yanayokidhi, uandishi wa kizamani unaweza silaha inayofaa
Waandishi wa Hong Kong Wapambana na Udhibiti wa Habari Unaofanywa na Vyombo vya Habari
Tovuti nne za habari zimetoa tamko la pamoja kulaani kitendo cha polisi kuwashambulia polisi kwa makusudi. Waandishi kadhaa wamekuwa wakidhitiwa na vyombo vya habari kwa hofu ya kuikasirisha Beijing.
Raia wa Guinea Waendelea Kuwa Wavumilivu Pamoja na Uwepo wa Ebola
Wakiwa wamenyanyapaliwa na jamii ya kimataifa, raia wa Guinea wanakabiliana vilivyo na changamoto za kila siku za maisha bila kujali hatari zilizopo, majonzi, pamoja na kutiliwa mashaka na jamii ya kimataifa.
Ungana nasi kwa Mkutano wa Global Voices Tunis Novemba 1

Ungana nasi kwenye mkutano wa Global Voices nchini Tunis Novemba 1, 2014 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana kwenye Maabara ya 404.
Siku ya Blogu Oktoba 16: Shiriki Mjadala wa #KutokuwepoUsawa katika Jamii
Iambie dunia kile unachodhani ndio maana ya kukosekana kwa usawa. Andika simulizi lako, waambie wengine mtazamo wako, jadili na jenga hoja, Fanya hivyo Alhamisi ya Oktoba 16, siku ya Maandimisho ya Blogu Duniani.
Kutangaza Mkutano wa Global Voices 2015 Utakaofanyikia Cebu, Ufilipino, Januari 24–25!
Mkutano wa Uandishi wa Kiraia wa Global Voices utafanyika Januari 24-26, 2015 jijini Cebu, Ufilipino. Jiandae kupata habari kamili!
Katika Picha: Gaza Yaadhimisha Eid Al-Adha
Ikiwa na zaidi ya Wapalestina 2,000 waliojeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Isralei katika Ukanda wa Gaza, raia bado wanaona leo hii kuna kila sababu ya kusherehekea sikukuu ya Kiislam ya Eid Al-Adha.