Kutangaza Mkutano wa Global Voices, Dar es Salaam, Novemba 2, 2014

gvswahili.jpg

Wanakundi wa timu ya Kiswahili waliohudhuria Mkutano wa GV Citizen Media, mwezi Julai, 2012. Mpigaji Picha: Paula Góes

Tunayo furaha kubwa kutangaza mkutano wa Global Voices unaotarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Tanzania, siku ya Jumapili, Novemba 2, 2014, kuanzia saa 6 mchana hadi saa 10 alasiri. Mkutano huo utafanyika kwenye Kituo cha Teknolojia na Mambo ya Jamii, KINU, washirika wa Global Voices Swahili nchini Tanzania.

Mikutano ya Global Voices ni mikusanyiko midogo inayokusudiwa kusaidia kuwaunganisha waandishi na watafsiri wa Global Voices na wasomaji pamoja na wadau wa habari za kiraia. Wakati mkutano huu ukifanyika, mikutano mengine itakuwa ikifanyika kwenye miji ya Accra, Beirut, Tunis, na Belgrade.

Mkutano huu wa Dar es Salaam ni fursa ya kwanza ya Global Voices kukutana na wasomaji wetu nchini Tanzania. Katika agenda za mkutano, kadhalika, kutakuwa na mada kuhusu Uandishi wa Kiraia Tanzania, itakayotolewa na Ndesanjo Macha, ambaye ni mwanablogu wa kwanza nchini Tanzania; namna ya kukusanya na kuandika kwa ajili ya wasomaji wa Kitanzania, itakayotolewa na Constantine Manda wa Vijana FM; na umuhimu wa kuandika katika lugha ya Kiswahili, itakayotolewa na Zamda Ramadharan, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Unaweza kuona agenda kamili za mkutano huo hapa.

Kama ungependa kushiriki, tafadhali jaza fomu ya kujiandikisha. Tukio hili liko wazi kwa wote ingawa nafasi ni chache sana.

Hapa, unaweza kuona ramani ya namna ya kufika kwenye Jengo la Conservation, lililo kwenye barabara ya Ali Hassani Mwinyi, karibu na ofisi za Airtel, Moroko, mahali utakapofanyikia mkutano.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: christianbwaya [at] gmail [dot] com

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.