Tunayo furaha kubwa kutagaza kwamba Mkutano Mkuu wa kiraia wa Global Voices 2015 utafanyika kati ya tarehe 24 na 25 Jijini Cebu, nchini Filipino.
Mkutano wa Sita wa Uandishi wa Kiraia unatupeleka kwa mara ya kwanza katika bara la Kusini Mashariki Asia, ambapo tutafanya majadiliano ya wazi pamoja na warsha kwa siku mbili na wanablogu, wanaharakati na wanateknolojia kuhusu hali ya uandishi wa kiraia, ushiriki wa mtandao wa intaneti ndani ya kuta Makao Makuu ya Jimbo la Cebu Jijini Cebu. Mkutano huu wa 2015, kama ilivyo mikutano mingine iliyopita, ni fursa ya kujifunza na kushirikishana uzoefu miongoni mwa jamii yenye sura ya kidunia.
Kaa mkao wa kula tunapojiandaa kuzindua touti ya Mkutano huo itakayokuwa na habari za kina kwa tukio, taarifa za usajili na zaidi -kuingiza siku hizo kwenye ratiba zako!