- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Katika Picha: Gaza Yaadhimisha Eid Al-Adha

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Palestina, Chakula, Dini, Uandishi wa Habari za Kiraia, Upiga Picha, Vita na Migogoro
Wapalestina wa Gaza wanasherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha kupitia kiungo habari #GazaEid na #غزة_بدها_تعيد (kikiwa na maana, Gaza yataka kusherehekea Idi). Picha hii iliyowekwa na Kituo cha Mawasiliano cha Palestina ikiwaonesha watoto wakiwa katika mtaa ulio na pilika pilika nyingi za watu wakifanya manunuzi [1]

Wapalestina wa Gaza washerehekea Eid Al Adha kupitia kiungo habari #GazaEid na #غزة_بدها_تعيد (ikiwa na maana, Gaya yahitaji Kusherehea Sikukuu ya Id). Picha hii iliyowekwa na Kituo cha Mawasiliano cha Palestina ikiwaonesha watoto wakiwa katika mtaa ulio na pilika pilika nyingi za watu wakifanya manunuzi

Kukiwa na zaidi ya raia wa Palestina 2,000 waliojeruhiwa [2] katika mashambulizi ya hivi karibuni yafanywayo na Israel katika ukanda wa Gaza, raia bado wana kila sababu ya kuadhimisha sikukuu ya Kiislam ya Eid Al-Adha [3], inayoanza leo miongoni mwa waislamu wengi duniani kote.

Eid Al Adha ama sherehe ya kutambika inahitimisha msimu wa Hajj [4], ambao, mwaka huu umewakutanisha mahujaji milioni 2 [5] kutoka nchi mbali mbali duniani.

Huko Gaza, bado kuna matumaini pamoja na kuwepo kwa rubble, uharibifu, pamoja na vifo. Watumiaji wa Twita walianza kusambaza picha zilizopigwa katika mitaa na masoko yaliyojaa watu na kisha kutuma jumbe za matumaini kwa kutumia kiungo habari#GazaEid [6] na #غزة_بدها_تعيد [7] (ikiwa na maana kuwa, Gaza yataka kusherehekea Eid).

Siku 50 za ukatili zilizogharimu maisha ya wapalestina zaidi ya 2,137, wengi wao walikuwa ni raia, miongoni mwao wakiwa ni watoto 577, na wengine 10,870 wakijeruhiwa, ingaliweza kuwa imeisambaratisha miundo mbinu ya ukanda wa Gaza lakini kilichoshindikana ni kuharibu ustaarabu wa raia, na ambao leo hii wanatikisa kifusi katika kusherehekea Idi.

shambuliio hili lilikuwa na madhara ya wazi kabisa katika uchumi wa Gaza, ikiwa ni pamoja na ukweli kuwa, ingalikuwa vigumu kwa miundo mbunu ya raia kutokuharibiwa: zaidi ya makazi 18,000 yaliharibiwa, ikiwa ni pamoja na shule 100, vituo vya afya 50 pamoja na kuharibiwa kwa hospitali 17 au 20 hivi kubomolewa kabisa.

Mtumiaji wa Twita, Sana'a Mohammed aweka picha ya mvulana aonekanaye akicheza katika uwanja ulioharibiwa kabisa:

Ilikuwa jana tu pale mpiga picha za kiraia, Omar ElQattaa alipopiga picha ya mwanaume aliyekuwa amebeba mbuzi kwa ajili ya kutoa sadaka:

Sayel akiwa Gaza, aweka picha ya mkusanyiko wa matukio mbalimbali ya maandalizi ya Idi:

zifuatazo ni picha nyingine kutoka kwa Hasan Mustafa za kutoka katika maduka mbalimbali huko Gaza zilizopigwa mapema wiki hii:

Na pia, hamasa ya sherehe ya Idi huchagizwa vizuri zaidi kwa And of course, Eid's spirit is always intensified by traditional, homemade ma'moul (date cookies) aina ya biskuti za kitamaduni zitengenezwazo majumbani:

Pamoja na machungu yote, watoto wataifurahia Id, anasema Hiba akiwa Gaza:

Mamoja na machingu yao, watoto wa Gaza watasherehekea Idi

Kutoka katika maduka ya Gaza, mahali ambapo hamasa inaonekana kuwa ya juu kabisa:

Gaza inahitaji kusherehekea Idi

Nuseiba aeleza bayana kuwa, bila kujali maisha ya watu yaliyopotea katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, jiji hili bado linakila sababu y kusherehekea sikuu ya Idi:

Mwaka huu sherehe ya utoaji sadaka imekuja mapema Gaza, ambapo sadaka ya watoto na mali ilitolewa. pamoja na masahibu yote haya, Gaza inahitaji kusherehekea Idi

Farah joins Nuseiba, pamoja na watumiaji wengine wengi wa Twita walitanabaisha kuwa, ,Idi iliyopita iliwakuta watu wa Gaza katika vita:

Kwa kweli, wanaweza: