Jiandikishe Sasa kwa Mkutano wa Global Voices 2015: Januari 24-25 jijini Cebu, Ufilipino

Cebu Provincial Capitol Building, Cebu City, venue for the Global Voices Summit 2015. From Wikimedia Commons. Photo by Allan Jay Quesada.

Jengo la Makao Makuu ya Jimbo la Cebu, Jijini Cebu, mahal patakapofanyika Mkutano Mkuu wa Global Voices 2015. Picha ya Wikimedia Commons. Picha imepigwa na Allan Jay Quesada.

Uandikishaji kwa ajili ya Mkutano Mkuu Uandishi wa Kiraia wa Global Voices 2015 sasa umefunguliwa!

Dhima ya mkutano wa 2015 ni “Mtandao huru wa Intaneti: Mtazamo wa kimahali, haki za Kidunia .” Washiriki kutoka nchi zaidi ya 70 watakusanyika kwenye jengo la Makao Makuu ya Jimbo la Cebu, jijini Cebu, nchini Ufilipino mnamo Januari 24-25, 2015 ili kusaili uhusiano kati ya mtandao huru wa intaneti, uhuru wa kujieleza na harakati za kiraia mtandaoni duniani kote. 

Tangu mwaka 2006, Mikutano ya Global Voices imewaleta pamaja wanaharakati wa kidijitali, wabunifu pamoja na jamii za uandishi wa kiraia kutoka duniani kote. Mikutano hii huanzisha urafiki mpya na kutengeneza mazingira ya kuzaliwa kwa mawazo na ushirikiano kutoka sehemu mbalimbali. Chakula kizuri, mitoko, utamaduni na sherehe hupata nafasi kwenye ratiba.

Jifunze zaidi kuhusiana na tukio hili, na jiandikishe hapa ili kuwa sehemu ya Mkutano huu wa kuadhimisha miaka kumi. 

Tunatarajia kukuona kwenye jiji la Cebu mwezi Januari!

Mkutano Mkuu wa Uandishi wa Kiraia 2015 umewezeshwa kwa ushirikiano wa Mfuko wa Ford Mfuko wa MacArthur, GoogleShirika la Open Society, Mfuko wa KnightYahoo!, kampeni ya Mtandao Tuutakao shirika la Making All Voices Count, na  Kituo cha Uandishi wa Kiuchuguzi cha Ufilipino.

1 maoni

 • Michael Fidelis

  Habari Ndugu,

  Naitwa Michael Fidelis ni mtanzania ninayeishi mjini Nairobi nchini Kenya ambaye napenda sana uenezaji wa habari/taarifa duniani kote katika nchi zinazozungumza na kujifunza lugha ya Kiswahili.

  Ningependa kushiriki nanyi katika uenezaji huu wa habari.

  Mwasiliano yangu ni: +254724720039.
  Baruapepe: dmikepresenter@gmail.com
  Facebook: D’ Mike Presenter.

  ASANTE.

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

 • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.