- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanabogu wa Togo Wamtania Rais Kufuatia Ujumbe wa Bango Barabarani

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Togo, Elimu, Habari Njema, Mawazo, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Upiga Picha, Utawala, Vichekesho, Vijana

Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi/a>”. Raia wa Togo waliguswa na kuvutiwa na ujumbe huo. Waliingia kwenye mtandao wa Twita kuchekeshana kuhusiana na bango hilo na kutengeneza alama habari #merciPapaFaure [1] (Asante sana Baba Faure). 

Sawa, vipi cheka kidogo na alama habari #mercipapaFaure ? 

Picha hiyo juu imesambaa mno kwenye mtandao wa Twita. Adzima anatoa maelezo kidogo kuhusu hali ya mambo ilivyo kwa watoto wa Togo [1]shuleni.