- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Video ya Kuonesha namna Mlima Ontake Ulivyolipuka

Mada za Habari: Asia Mashariki, Japan, Habari za Hivi Punde, Majanga, Michezo, Safari, Uandishi wa Habari za Kiraia

Mtu mmoja amethibitika kufariki dunia [1], na takribani wakwea mlima wengine hamsini wamejeruhiwa, na wengine kumi hawajulikani walipo baada ya Mlima Ontake (御嶽山), eneo maarufu la ukweaji wa milima katikati ya Japan, umelipuka kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano. Habari za tukio hilo zinaonesha wingu zito la majivu, na sehemu ya juu kwenye kilele cha mlima huo ikiwa imefunikiwa na tope zito la kijivu.

Search for Ontake kwenye mtandao wa Twita [2] kufuatilia habari zinazoendelea kuhusu tukio hili.

Mtumiaji wa mtandao wa YouTube  kuroda terutoshi [3] aliweka kipande kidogo cha video chenye picha zinazotisha alichokirekodi kwa kutumia simu yake ya mkononi kuonesha mlipuko wa mwanzo ulivyotokea kwenye kilele cha mlima huo. “Tuondoke hapa!” anasema, wakati wingu hilo la majivu likiwashukia watu waliokuwa wakikwea mlima.

Mlipuko mkubwa kwenye Mlima Ontake

Shirika la Habari la AP liliweza kupata picha za wakwea mlima waliokuwa na hofu kubwa huku wakiharakisha kushuka mlima [4].

Mlima Ontake wenye urefu wa meta 3,067 , ni mlima wenye volkano, wa pili kwa urefu nchini Japani baada ya Mlima Fuji. Unapatikana kwenye eneo la Gifu, karibu na jiji kubwa la Nagoya katikati ya Japani, na ni maarufu kwa upandaji mlima hasa nyakati za majira ya joto na kipupwe.

Kwa sababu ya kukosekana kwa watu wengi na wengineo kujeruhiwa, watu wengi wanatafuta habari kuhusu hali na maendeleo ya marafiki na wapenzi wao waliokwama kwenye mlima huo wakati wa mlipuko.

Twiti moja maarufu inaonesha hali ilivyo kwa kutumia ramani yenye mchoro:

 Jamii ya wakwea mlima wa Japani ni kundi la watu wenye ukaribu mkubwa ambao mara nyingi huwasiliana kwenye mtandao wa kijamii, ikiwa ni pamoja na mtandao wa Twita. Kwa hiyo, watu wengi wana wasiwasi na wanatafuta habari zaidi.

Idara ya moto imethibitisha mwanamke mmoja alifariki dunia kwenye Mlipuko wa mlima Ontake

Hatua hii inakuja siku moja baadae baada ya mpanda mlima maarafu kutoka Tajimi huko Gifu akiwa ameweka picha nzuri kutoka kwenye kilele cha mlima Ontake:

Nilitumia siku nzuri kwa kukwea mlima mpaka kwenye kilele cha Mlima wa Ontake

Mpaka sasa, hafahamiki aliko.

 

Update

Jitihada za uokoaji zinaendelea kuwatafuta wakwea mlima waliokwama kwenye kilele cha mlima huo, ambao bado unaendelea kulipuka.

 

Featured image courtesy kuroda terutoshi [3]