- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uimarishaji wa Amani ya Kudumu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Dini, Elimu, Habari Njema, Harakati za Mtandaoni, Mahusiano ya Kimataifa, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Utawala, Vita na Migogoro

Wakati Umoja wa Mataifa ukizindua mpango wake wa kulinda amani kwa kutuma wanajeshi 1,500 [1] nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wafuatiliaji wachache wanajiuliza ni kwa nini uamuzi huu ulichukua muda mrefu [2] pamoja na kuwepo kwa wahanga wengi wa machafuko. Les Cercles nationaux de Réflexion sur la Jeunesse (CNRJ) ni shirika lisilo la kiserikali mjini Bangui , Jamhuri ya Afrika ya Kati, linalojibidisha katika kuimarisha msingi wa amani ya kudumu [3] nchini humo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Bangui. Ifuatayo ni video inayoonesha kwa kina kile kinachoendelea katika mkakati huu: