Surprising Europe: Mkusanyiko Huru wa Simulizi za Uhamiaji

Screenshot from Episode 09 "Home Sweet Home." "Evariste has returned to Burkina Faso after working in Italy. Now he feels free and is happy again."

Picha iliyopigwa kutoka katika sehemu ya 9 “Nyumbani Patamu Nyumbani.” “Evariste yupo Burkina Faso kwa sasa, hii ni baada ya kufanya kazi nchini Italia.Anajisikia kuwa huru na mwenye furaha”

Wapo mamilioni ya watu kama hawa. Wanaishi maeneo mbalimbali katika bara letu la Ulaya. Wote hawa, wamewekwa katika kundi la wahamiaji Pamoja na hali hii, kila mmoja ana simulizi yake iliyo tofuti na ya wengine. Kwa maana hii, kama tungetaka kuelezea historia ya maisha ya kila mmoja, ingelitulazimu kuandaa maelfu ya vitabu.
Hata hivyo, kuna mradi wa mtandaoni unaosaidia kupata mawasiliano na watu hawa ambao kiujumla wanatambulika kama wahamiaji. Unasaidia kukabiliana na na unyanyasaji na udhalilishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea watu ufahamu zaidi kuhusiana na watu hao. Surprising Europe  ni kwa ajili yao, ni kitabu kilicho huru, kilichoandikwa na watu wengi na kilichohanikizwa kwa picha na video. Simulizi binafsi za watu, mafanikio, kukosa mafaninikio na matumaini, vyote “vinaandikwa” katika jukwaa hili. Ni wahamiaji wenyewe ndio wanaoelezea simulizi zao.

Inashangaza pale unapobaini ni ujasiri kiasi unaotakiwa katika kukabiliana na changamoto ya lugha, urasimu pamoja na mahusiano. Inashangaza pale unapoabaini kuna wengi wanaotaka kurudi makwao lakini wanashindwa. Wengi wanarudi nyumbani na kuwaambia marafiki zao: ni bora kuujengea mustakabali wa maisha yetu tukiwa nchini mwetu. Inashangaza pale ujumbe huu unaposambazwa: ni bora kuwa masikini lakini mtu awe huru. Inashangaza pale unapogundua kuwa kumbe hata Ulaya kuna watu masikini na hata pale mtu atakaposhuhudia kuwa bara hili la mda mrefu siyo pepo waliyokuwa wakiiwazia.

Na pia, inashangaza, kwa upande mwingine, pale mtu anapoona kuwa ndoto zake zimekamilika, And it is surprising when, on the contrary, someone sees their dream come true, wale waliofaninikwa kupia mziki, wale waliojijengea ujuzi viwandani, wale waliosoma na kuweza kujiajiri. Katika jukwaa hili huru, simulizi hazifupishwi, na uzoefu unabaki kuwa ni urithi wa kila mmoja. Tovuti hii itajumuisha simulizi za changamoto katika jamii na pia mafanikio. Unapaswa kujiunga na mtandao huu bila ya kuwa na mategemeo fulani, bila ya kukisia kile utakacho kikuta, kama jinsi ukutanavyo na marafiki, pale mada moja inavyopelekea kutokea kwa mada nyingine.

Wazo hili la mradi usio wa kimaslahi umelenga kuweka kumbukumbu ya uhalisia wa hali kwa wahamiaji haramu na pia wale waishio kihalali. Mradi huu umebuniwa na Witfilm Amsterdam na Ssuuna Goloob, waliofika barani Ulaya kutoka Uganda ili kujionea wao wenyewe kama ni kweli kwa kile alichokuwa akikisikia kuhusiana na nchi zetu na jinsi tunavyoishi. Mradi ambao wengi wanauamini, wakiupima kwa kuzingatia wafadhili wake: Kutoka Al Jazeera, hadi Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, hadi Shirika la Kimataifa la Uhamiaji pamoja na Mfuko wa Umoja wa Ulaya wa Urudishaji wa Wahamiaji Makwao.

Haikuwa bahati tu kwa wazo hili kuibuliwa huko Amsterdam, mji mkuu wa Uholanzi, Hii ni kwa sababu jiji hili kwa sasa, linachukuliwa kuwa ni moja ya majiji yaliyo na idadi kubwa ya wakazi walio na utaifa tofauti: wakazi 176 kati ya jumla ya wakazi 811,000 (Kwa upande mwingine, eneo la mji mkuu lina wakazi milioni 1.6).

Tovuti hii imegawanywa katika makundi 6: Kwenda kuishi Ulaya, Maisha ya Ulaya, Short on luck, Kufanya Kazi, Kurudi Nyumbani, Mziki. Mradi ndani ya mradi ni aina fulani ya mfululizo wa vipindi vya runinga. Kila kipindi kikiwa ni tofauti na kingine lakini vikiwa vinafanana kwa kwa maudhui. Simulizi za kukata tamaa, lakini pia, simulizi amabazo zinaweza kuibua hamasa, tumaini na ubunifu. Upande wa taabu na upande wa mafanikio. Mapambano, wakati mwingine makabiliano, mafaniniko mara nyingi. Wahusika halisi ndio waliojitokeza katika mfululizo wa makala hizi za runinga ambazo zimeshaoneshwa Al Jazeera na pia katika runinga ya Taifa ya Uholanzi. Kwa utaratibu huu, wanajaribu pia kuepukana na vikwazo vya mitandaoni, tafsiri pamoja na mitazamo ya watu.
Mradi huu pia una wimbo maalum, “Surprising Europe”. Umeimbwa na Annie, ambaye ni mzaliwa wa nchini Italia, akiwa na asili ya nchini Liberia. Mwanadada huyu angependa kurudi nchini Liberia. Anataka arudi huko kwa lengo la kuiona nchi yake au labda kuishi huko. Kwa sasa, Annie ni miongoni mwa wanakikundi “mchanganyiko” wa Bendi ya Afro, Pepe Soup. Wanataka kuufikishia ulimwengu ujumbe: UNGANENI!

Surprising Europe ni ya wahamiaji, lakini pia, inamhusu mwingine yeyote apendaye kupata ufahamu wa kutosha na kuwafahamu hawa wahamiaji. Na ngalao kufahamu kwa undani zaidi kuhusu maisha yao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.