- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Nzige Wavamia Mji Mkuu wa Madagaska

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Afya, Chakula, Habari za Hivi Punde, Harakati za Mtandaoni, Majanga, Mazingira, Sayansi, Uandishi wa Habari za Kiraia

Watumiaji-mtandao wa Twita na Facebook kutoka mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wamepachika picha kadhaa za nzige wakivamia mji. Uvamizi wa nzige sio tukio la ajabu nchini Madagaska, hasa baada ya dhoruba za kitropiki, lakini sio kawaida katika miji mikubwa. Nzige wanaweza kuwa na madhara makubwa kwa mazao, hasa katika nchi ambayo imekumbana na baa la njaa katika miaka iliyopita.