- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino

Mada za Habari: Asia Mashariki, Ufilipino, Afya, Habari za wenyeji, Historia, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

philippine_health_research [1]Ikiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health [2]) inalenga kuweka kumbukumbu [3] na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo.

Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili kutoka porini katika kujikinga au kujitibu magonjwa yao. Lakini uharibifu wa mazingira na kushambuliwa vikali na tamaduni kuu za jamii zinazoishi mabondeni hivi sasa kunatishia mila hizo za tiba.