- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuhoji Kimya cha Vyombo vya Habari Siku za Wikiendi Kuhusu Habari za Ebola

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Guinea, Liberia, Naijeria, Sierra Leone, Afya, Uandishi wa Habari za Kiraia

“Ni lini Habari za Ebola zitatangazwa kwa masaa 24 siku saba za wiki?,” anauliza [1] Profesa Crawford Kilian wa Marekani na Kanada:

Nimezoea kusikia habari mpya zikisitishwa kutangazwa nyakati za wikiendi. Vyombo vya habari, mashirika ya serikali, Asasi za Kiraia vyote vikiishia kutangaza habari siku ya Ijumaa mchana na kuibukia siku ya Jumapili asubuhi kwa mara nyingine.

Lakini baada ya majuma kadhaa ya Ebola, ninapoteza uvumilivu na jamaa wanaoishi kwa kutangaza habari za maradhi ya Ebola. Ndio, ni sawa kwao kwa makubaliano yao ya pamoja yanayowapa masaa manane kwa siku, bila kujumuisha wikiendi, siku za mapumziko na manufaa bora ya kiafya. 

Lakini kama Ebola haikubaliki kama anavyosema Dk Chan, vipi kuhusu kutafuta fedha za kuwalipa hawa jamaa kutumia muda wa ziada ili habari za ebola ziendelee kutangazwa hata muda wa Wikiendi (bila kutaja siku za mapumziko)? Unaweza kuona mazingira ambayo habari za Pearl Harbor zinasubiri mpaka mwandishi mmoja aje na ahabari zake siku za Jumatatu, Desemba 8, 1941? Au habari za kifo cha JFK zisitanagzwe mpaka siku ya Jumatatu inayofuata ya Novemba 25, 1963?

Lakini vyombo vya habari vya Afrika Magharibi, ukiacha vichache, vimekuwa vikipotea kuanzia siku ya Ijumaa mchana, na kuzinduka muda wowote siku za Jumatatu. Ndivyo yanavyofanya Mashirika kama WHO na mashirika mengine ya afya. Ninajua vizuri sana kwamba wanahangaika na kukosekana kwa mafungu ya fedha kutoka serikalini na hivuo vinafikiri nidhamu ya matumizi ni njia pekee ya kukabiliana na mdodoro wa mwaka 2008.