Kimbia! Waislamu Wanakuja!

Na Sami Shah

Nyie Waislamu, ni watu wa ajabu sana. Lakini sasa ni watu wa ajabu kwa namna gani? Hilo ndilo swali kubwa siku za leo.

Kadri makundi kama vile ISIS/ISIL/IS/FuckNutBuggerFucks yanavyoendelea kuandamana kwenye maeneo mengi kama Iraq/Levant/Babylonia/Assyria, na shughuli nyingine zenye kutiwa ujasiri wa kipuuzi zinazoendelea duniani kote kwa kuchochewa na matamshi ya kijinga yanayotolewa kwenye mitandao kama You Tube na kuhamasisha watu kukatwa vichwa na watu wanaojituma wenyewe kufanya hivyo, mambo yataendelea kuwa magumu kwa Waislamu wa kawaida.

Sami Shah. Used with permission.

Sami Shah. Imetumiwa kwa ruhusa.

Lakini Sami, nakusikia unavyouliza, “una maana gani unaposema mwislamu wa kawaida”? Je, yule jamaa anayevaa kibaghalashia huku akiwa kabeba gobore na mfuko uliojaa vichwa vya watu ndio “mwislamu wa kawaida”? Au ni yule mtu mwuungwana anayeishi mlango wa pili, mwenye watoto watatu na mke mzuri? Tunawatambuaje? Tunawawekaje kwenye makundi yao? Tunawashindaje tunapopigana nao? Tunawezaje kuwazuia wasijiunge kuwa kundi moja kubwa na hatari la Kiislam?

Siwezi kuwa na majawabu yote, lakini ninaweza kusaidia kupitia baadhi ya maswali uliyonayo. Kwa hiyo, bila kuchelewesha muda (na kelele na kujisifu kusikohitajika), naomba nikuoneshe sehemu ndogo niliyoitoa kwenye kitabu changu I, MIGRANT [MIE, MHAMIAJI] ambacho kinajibu maswali yako yote.

Aina za Waislamu

(hii inakwenda vizuri kama utaisoma kwa lafudhi ya mtangazaji wa Kiingereza David Attenborough)

Waislamu Waungwana:

Wazazi wangu ni mfano mzuri wa aina hii ya waumini. Wanamwamini Allah, kitabu kitakatifu cha Quran na Mtume Muhammad. Wote waliswali swala tano kwa siku, walitoa sadaka kwa maskini, walikwenda Hija na walikuwa na walithamini sana kuomba rehma za Mwenyezi Mungu, Allah. Wote mama na baba yangu wanafahamu aya za Quran kwa moyo, hasa zile zilizosaidia kutafuta kitu kilichopotea, na kwa ujumla walijisikia fahari kuwa Waislamu. Mama havai hijab na mama hajafuga madevu. Na wala hawafikiri kwamba Nchi za Magharibi ndizo zilizomtengeneza Sheitwan na kwamba raia wa Kimagharibi ndio wanaopaswa kupigwa na kuangamizwa kwa kutumia matendo ya kujitoa mhanga yanayosukwa kwa ustadi na kwa kushtukiza.

Hata hivyo, wanafikiri kwamba Marekani inawachukia Waislam, kiasi kwamba kitendo chake cha kuikumbatia Israel ni ushahidi wa hili, kwa uthibitisho wa kuzivamia nchi za Afghanistan na Iraq. Haya ni maoni yao na, kwa kiasi kikubwa, hayana sumu wala hayaathiri mazingira ukiachilia imani ya mama yangu kwamba wanaume wote ni wavivu na ile ya baba yangu kwamba wanawake wote hutoa ushauri usio na kichwa wala miguu.

Uwezekano ni kwamba, kama ungewatafuta Waislamu mia moja kwa njia ya nakisi duniani, wote wangekuwa kama wazazi wangu. Uislamu ni sehemu ya maisha yao, lakini huwa haiwi kama ilivyotarajiwa.

Waislamu Wazembe:

Kwa kuhukumiwa vibaya na makundi yote ya Waislamu, hawa ni kundi linalojulikana zaidi. Ni Waislamu kwa kuzaliwa na kwa jina. Wanaweza kwenda mbali zaidi kwa kukubaliana na masuala ya utakatifu wa Quran, Allah na Mtume wake, lakini hiyo huishia hapo. Hawa hawana subira kwa kutekeleza ibada na kwa ujumla ni wagumu kujitambulisha hadharani kama Waislamu.

Baadhi yao ni walevi, hata kama wanajua pombe ni haramu kidini. Lakini hawali nyama ya nguruwe. Nguruwe ni haramu kabisa kwa Mwislamu. Ni kweli, wengi wa kundi hili, wanaweza kuutamani mnofu wa nguruwe ikitokea wameuona, na hata wanaweza kusimama na kuangalia uwezekano wa kupata japo mbavu tu baada ya kuona tangazo kwenye runinga, lakini kwa kawaida mahali salama zaidi kuishi kwa nguruwe ni kwenye nchi ya Kiislamu [maana kamwe hataliwa]. Kuhusu pombe, kuna kila aina ya uhalalishaji unaotolewa na hawa jamaa. “Quran inazuia aina fulani za kilevi,” wanaweza kusema, wakionesha uharamu wa wazi wazi uliotamkwa kuhusu kilevi cha mvinyo uliotengenezwa kwa tende zilizochachuka. Au “Uislamu ni kwenda na wakati,” unaweza kusikia wakijitetea wakati wakigida mvinyo mkali kama vodka.

Kama ni mchoro wa maduara mawili yanayoingiliana mahali fulani kuonesha jinsi Waislamu wema na Wabaya wanavyofanana, mwingiliano ungekuwa kwenye imani kwamba Marekani inawachukia Waislamu, kwa ushahidi wa kuiunga mkono Israel , na hata kitendo chake cha kuivamia Afghanistan na Iraq.

Waislamu wa Ajabu:

Kwa sasa wamejichomeka kwenye kila fursa ya ajira serikalini katika nchi za Kiislamu unazoweza kuzifuatilia, jina jingine kwa aina hii ya Waislamu ni “Wapumbavu wanafiki”.

Hawa ni tofauti na Waislamu wazembe kwa kuwa, wanaweza kufanya kila aina ya dhambi na kuvunja kila kilicho haramu kwenye dini, lakini bado wanajifanya kuwa ndio alama ya Uislam. Unaweza kuwatambua kwa hisia za hasira wanazoonesha kwa eti kuipenda dini yao. Wanaume wanakuwa na madevu marefu, yanayotumika kuonesha misimamo yao ya kidini pamoja na mfumo dume; siku zote wana sehemu ya kipaji cha uso iliyosagika, kuonesha kwamba siku zote wanaswali sala tano. Wanawake huvaa hijab –haibani kama ilivyo kawaida, ila kujifunika gubigubi kinyume cha kanuni za fizikia na hata mitindo.

Muda wote utawaona wamebeba tasbiri yenye vifundo vya kufanyia maombi na haibanduki vidoleni. Kila ombi linaloombwa linafanyika kwa jinsia zote na kila Hija iliyofanyika. Wanaweza kushika dini kiasi cha kuachana na pombe na wanaweza kuwa waume na wake wema. Lakini wanaweka fedha mbele na wanaweza kuwalisha watu nyama ya nguruwe na mapaja yake yaliyokaushwa wakati wa kufunga ndoa na makafiri na pia wanaweza kula kiapo kwa jina la Sheitwani.

Hawa pia wanahesabika kwenye kundi la watu wanaoamini kwamba Marekani inawachukiwa Waislamu, na kwamba kitendo cha nchi hiyo kupenda kuikumbatia Israel ni ushahidi wa hili, kwa kujumlisha pia kitendo chake cha kuivamia Afghanistan na Iraq. Tofauti pekee kwa hawa ni kwamba wengi wao wanaweza kushirikiana na adui kama adui huyo atafika bei yao. Ukweli, hiyo si kweli. Si kama adui atafika bei –ni kama kuna bei  yoyote imetolewa.

Waislam Tishio:

Wanapenda kuzungumzia “Jihad” sana. Mfano mzuri ni imam wako wa Msikiti. Kwa mwonekano hawana tofauti sana na “Waislam wa ajabu”, tofauti yao ni uumini uliovuka mipaka. Wanaume si tu wamefuga madevu pia wamenyoa masharubu pia. Mtindo huu una mizizi yake kwenye imani kwamba Mtume alinyoa ndevu zake namna hiyo, ingawa hakuna ushahidi wa hilo. Na wala hakuna ushahidi kwamba alivaa suruari fupi mithili ya kaptula ndefu, lakini mitindo hiyo ndiyo maarufu zaidi kwa kundi hili.
Sasa ni vyema nitoe ufafanuzi kuhusiana na kundi hili la Waislamu. Waislamu Tishio wanaweza kusema “Jihad” zaidi na wanazungumzia kupambana na nchi za Magharibi na namna umma wa Waslamu unavyohitaji kuamka na kufanya mapinduzi, lakini uwezekano ni kwamba hutawakuta kokote kwenye mstari wa mbele.

Wamewekwa kwenye fungu la Kutisha, kwa kweli, na wazungu wanaona yanayofanywa na magaidi kwa sura yao. Kwa Waislamu wenzao, kundi hili ni linakera zaidi na linaonekana kuwa la kijinga zaidi. Tunawavumilia kwa sababu kwa wastani lina umuhimu katika kuwafundisha watoto wako Quran (almuradi unafuatilia kwa makini kuhakikisha kwamba elimu hiyo inabaki kuwa ya kukariri Kiarabu na haijumuishi maoni itikadi nyinginezo za kidini zilizojaa maoni). Maoni yao huanzia kwenye imani za kuzusha mambo –mfano kuamini kwamba madhehebu mengine nje yao yanapanga kuwaangusha –hadi kwenye imani kwamba Marekani inawachukia Waislamu, na kwamba kitendo cha nchi hiyo kuikumbatia Israel ni ushahidi wa hili, na zaidi uvamizi wa Afghanistan na Iraq. Mfano wa Waislamu wa Kutisha ni nchi yote ya Saudi Arabia.

Waislamu Wajinga Kabisa:

Wanaamini Marekani inawachukia Waislamu, na kwamba kitendo chake cha kuikumbatia Israel ni ushahidi, ukijumlisha na uvamizi wake kwa nchi za Afghanistan na Iraq. Tofauti pekee ni, wanataka kufanya kitu kurekebisha mambo. Na kitu wanachotaka kukifanya ni pamoja na kuwaua raia wa Nchi za Magharibi, kuwaua wanaounga mkono vitendo vinavyofanywa na nchi za Magharibi, kuwaua wanaounga mkono kichini chini vitendo vya Magharibi, kumwua yeyote aliyekinyume na vitendo vya kuwaua washirika wa wazi na wa siri wa Magharibi, na mwishowe nia ni kumwua yeyote. Mifano ya Waislamu Wajinga Kabisa ni Osama Bin Laden, Ayman Al Zwahiri, Al Qaeda wote, na wanamgambo wa Taliban.

Sami Shah ni mchekeshaji, mchoraji, mbunifu wa picha na mwandishi wa safu anayeishi Magharibi mwa Australia. Kazi zake zimewahi kuonekana kwenye majarida kama  New York Times, Comedy Central, NPR’s The World na Laughspin Magazine, na amefanya maonesho kwenye Mtandao wa Asia wa BBC na kwa TEDx Melbourne. Sami ni mwandishi wa MIE, MHAMIAJI: Safari ya Mchekeshaji Kutoka Karachi kwenda Nyikani

6 maoni

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> Christian Bwaya

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.