Video ya pili ikoneshayo mauaji ya kukatwa kichwa mwandishi wa habari wa Marekani, mauaji yaliyofanywa na dola ya Kiislam ya Raq na Syria(ISIS), dola iliyo na chimbuko lake kutoka kwenye kundi la Al Qaeda, kundi lililofanikiwa kutawala theluthi moja ya nchi ya Syria na robo ya nchi ya Iraq.
Video hii ya dakika tatu inadaiwa kuonesha kukatwa kichwa kwa Steven Sotloff, ambaye amekuwa akifanya kazi sehemu hatari katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati kama vile Bahrain, Syria, Egypt, Libya na Uturuki.
Sotloff hakuonekana kuanzia mwezi wa Agosti mwaka jana akipasha habari kutoka Syria.
Video hii ya kutisha inakuja mara baada ya ile ya kuchinjwa kwa mwandishi wa kimarekani wa habari katika picha, James Wright Foley, ambaye hakuonekana nchini Syria kwa siku 636, kabla ya video iliyoonesha mauaji yake kuwekwa hadharani na ISIS mnamo August, 19.
Sotloff alitambulishwa katika video ya Foley, angalizo likitolewa kuwa, yeye ndiye atakayefuatia. Kwa mara nyingine tena, mateka mwingine, David Haines, raia kutoka Uingereza, inasemekana amejitokeza katika video hii.
DC-based journalist Zaid Benjamin aliye na masjani yake huko DC, atwiti kwa mashabiki wake wanaofikia 45.5K:
Sauti ya mtu yule yule aliyejitokeza wakati wa mauaji ya Foley yatanabaisha kuwa, David Haines kutoka Uingereza ndiye atakayefuata.
— Zaid Benjamin (@zaidbenjamin) Septemba 2, 2014
#ISIS yatoa onyo kupitia video ya kukatwa kichwa kwa Steven Sotloff kuwa, mataifa mengine kamwe yasiiunge mkono Marekani.
— Zaid Benjamin (@zaidbenjamin) Septemba 2, 2014
Kwa mujibu wa NBC News, Haines, aliyekuwa mmoja wa wanajeshi wa Uingereza, aliachana na jeshi na kufanya kazi na mashiririka yasiyo ya kiserikali, ambapo alifanya kazi za kulinda usalama.
Mshituko
Wengi waliipokea habari hii kwa mshituko.
Ruwayda Mustafah, ambaye ni Mkurdi Mwingereza, akiwa na watu 41K wanaomfuatilia katika mtandao wa Twita, alishikwa na butwaa:
#ISIS yatoa taarifa ya kumkata kichwa Steven Sotloff —Ni nani angeweza kusema? Kukemewa vikali kumeonekana kupuuzwa na #ISIS
— Ruwayda Mustafah (@RuwaydaMustafah) Septemba 2, 2014
Emile Hokayem, mchambuzi wa masuala ya Mashariki ya Kati katika Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo mkakati, alitoa ufafanuzi katika ukurasa wake wa Twita ulio na wafuatiliaji 15k akisema kuwa kuzagaa kwa video za kutisha za namna hii zikionesha madhambi yafanywayo na ISIS inazifanya jamii za Mashariki ya Kati kuchukulia matukio haya kuwa ni kawaida.Mideast analyst at the International Institute for Strategic Studies, explains to his 15K followers on Twitter saying the widespread of such horrific videos showcasing ISIS’ crimes desensitize Middle Eastern societies:
Changamoto inayowakabili watu wa Mashariki ya Kati:Big danger hovering over Middle Eastern societies: Kadiri ya matukio ya kikatili yanavyoongezeka, Kupuuzwa kwa matukio haya kunachukuliwa kawaida katika maisha ya kila siku. Pumzika kwa amani Steven.
— Emile Hokayem (@emile_hokayem) September 2, 2014
Aliendelea kufafanua kuwa, ISIS ipo makaini kusambaza video hizi ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa “kuwatisha” watu.
Tofauti kati ya ukatili wa ISIS/Assad sio kwenye uasili bali katika kujitangaza: Kwa upande wa ISIS, makakati wao ni kutisha; Assad anahitaji mapingamizi.
— Emile Hokayem (@emile_hokayem) September 2, 2014
Washirika wake watuma salamu zao za rambirambi
Katika kurasa za Twita, wengi wamuelezea Sotloff kuwa ni mwandishi wa habari aliyekuwa makini.
Mwandishi wa habari katika picha, Mazen Mahdi kutoka Bahrain aeleza:
Tangu mapema, sikupenda sana kusema jambo kumhusu Steven Sotloff, lakini kwa yeyote aliyewahi kufanya kazi naye alitambua kuwa Steven Sotloff alikuwa mwandishi asiye kuwa na hofu kabisa. Pumzika kwa amani.
— Mazen Mahdi (@MazenMahdi) September 2, 2014
Anaongeza:
Kama wajinga hawa wa #isil, wangalijaribu kumfahamu Steven Sotloff, wangalitambua kuwa alikuwa akihabarisha masaibu halisi yanayowakumba watu.
— Mazen Mahdi (@MazenMahdi) September 2, 2014
Mwandishi wa habari, Portia Walker alalama kufuatia kifo cha mwandishi huyu:
Ninakuwaza Steven. Mwandishi mashuhuri, mpasha habari makini, na rafiki mwema.
— Portia Walker (@portia_walker) Septemba 2, 2014
Kwa mara ya mwisho, Lauren Bohn alikutana na Sotloff jijini Cairo. Mwandishhi wa habari huyu asiye na mipakaThe multi-media journalist, ambaye kwa sasa yupo Istanbul, anakumbusha kuwarecalls:
Katika mgahawa waAt a smoky cafe jijini Cairo, akiwa anachapa katika vitufe vya simu yake, tapping on his keyboard, akitupa mawasiliano yake pamoja na tabasamu zurisharing contacts + smiling widely. Hii ilikuwa ndio mara yangu ya mwisho kumuona Steven. Ni kumbukumbu ya kipekee. Pumzika kwa amani.
— Lauren Bohn (@LaurenBohn) Septemba 2, 2014
Na mwaandishi wa Global Post, Jeb Boone alikutana na Sofloff nchini Yemen. Anakumbuka namna watu walivyokuwa wakishindwa kuwatofautisha:
Nilikutana na Steven nchini Yemen. Watu walishindwa kututofautisha kwa kuwa sote tulikuwa wanene na weupe. Ilifurahisha kwa kweli. Pumzika kwa amani rafiki.
— Jeb Boone (@JebBoone) Septemba 2, 2014
#KuzuiwakwavyanzovyahabarivyaISIS
Kama ilivyokuwa kwa video ya Foley, wengi wanashinikiza habari za ISIS kuzuiwa. Badala ya kusambaza video ya ISIS ya mauaji ya kumkata mtu kichwa, watu wanawataka watu waomboleze kifo cha Sotloff kwa kumkumbuka kwa mazuri aliyoyafanya wakati wa uhai wake.
Miongoni mwao ni Zach Green, ambaye anasema:
Video ya
Don't share #ISIS ya uuaji kwa kukata kichwa, Hiki ndicho wanachokitaka. #ISISmediaBlackout Pumzika kwa amani Steven Sotloff. pic.twitter.com/c3gDLTbBar
— Zach Green (@140elect) September 2, 2014
Tangu kuandikwa kwa Twiti hii, imeshasambazwa mara 800.
Kutoka Libya, Ismael atoa mchango wake:
#ISISmediaBlackout pic.twitter.com/8rynuislyS
— Ismael (@ChangeInLibya) September 2, 2014
Boone aongeza:
Siwezi kuamini kuwa usambazaji wa video hizi bado unaendelea lakini haifai kwa mtu kuwaunga mkono ISIS kwa kusambaza video hizi. Pumzika kwa amani Sotloff.
— Jeb Boone (@JebBoone) Septemba 2, 2014
Na kutoka Lebanon, Elie Fares aelezea:
Usiwape kile wanachokihitaji: Siyo kwa kusikiliza & wala kutazama ukatili wao wenye lengo la kutisha watu. #ISISMediaBlackout pic.twitter.com/9H7Zf9q6dQ
— Elie Fares (@eliefares) Septemba 2, 2014
Kipi kinafuata?
Joshua Hersh, mwandishi wa habari anayeripotia Huffington Post Middle East aliye na maskanni yake New York, anasema kuwa, kuna juhudi hafifu kabisa katika kukabiliana na ukatili unaofanywa na ISIS:
Inaonekana kuwa ISIS ndilo kundi pekee duniani linaloamini kuwa Obama atumia njia za kimabavu kukabiliana na ISIS.
— Joshua Hersh (@joshuahersh) Septemba 2, 2014
Wakati haya yakiendelea..
Raia wa Syria, Razan Saffour anatukumbusha kuwa, hata waandishi wa habari wa Kiislam hawasalimiki wawapo mikononi mwa ISIS.
Wiki mbili zilizopita, ISIS walimuua mwanahabari mwislam wa Syria, Bassam Raies. Jumuia za kimataifa wala hazikulaani kitendo hicho. #Syria pic.twitter.com/Obms6gTiuK
— Razan Saffour (@RazanSpeaks) Septemba 2, 2014
1 maoni
pumzika kwa amani kamanda Mungu atakulipa sawa sawa na matendo yako