Blogu Sita za Kiingereza Zinazoweza Kukusaidia Kuielewa Japani

Photo by Flickr user Taro Yamamoto. CC BY-NC-SA 2.0

Picha na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Taro Yamamoto. CC BY-NC-SA 2.0

Ukilinganisha na muongo uliopita, kabla ya Facebook, Twita na mitandao mingine ya kijamii haijatwaa nafasi, hivi sasa hakuna blogu nyingi za ki-Japan kama ilivyokuwa.

Zipo chache zilizobaki. Kama unahitaji kukuza uelewa wa kina kuhusu Japan, blogu hizi ambazo nyingi zimeandikwa na watu waliobobea, ni uwanja mzuri wa kuanzia.

Blogu ya SNA – Shirika la Habari la Shingestu

Ikiwa zaidi ya blogu, Shingetsu ni shirika huru la habari ambalo huweka habari mpya za mara kwa mara pamoja na uchambuzi kuhusu matukio yanayotokea Japan. Ikiongozwa na mwandishi wa habari Michael Penn, mchangiaji wa Al-Jazeerawa mara kwa mara, Anwani ya Twita ya SNA ni namna nzuri ya kubaki kuwa kinara wa kutangaza habari zinazotokea nchini Japani.

Shisaku

Kama unataka kupata uelewa mzuri wa siasa za Japani, Shisaku ni mahali sahihi pa kuanzia.

Ikiandikwa na mwanazuoni na mchambuzi  Michael Cucek, mkazi wa Wilaya ya Mjini Tokyo tangu mwaka 1994, Blogu ya Shisaku inajaribu kuwatambua watu maarufu na makundi yanayoongoza mwelekeo wa siasa za Japani, na wakati mwingine hutoa mtazamo wa kiweledi kuhusu matukio yanayotokea.

Mahali pazuri kuanzia ni kwenye post hii ya blogu hiyo inayoeleza kwa kina upuuzi nyuma ya mtazamo wa kiudanganyifu wa Kijapani.

Blogu ya Tokyo Reporter

Ikianzia ilikoishia blogu ya zamani nzuri (na sasa imefungiwa) Tokyo Confidential, Tokyo Reporter inatoa mhutasari wa habari zinazoandikwa na magazeti ya wiki yanayoandikwa nchini Japani.

Ikiwa na habari nyingi za ngono, na kiasi fulani cha habari za matumizi ya nguvu, blogu ya NSFW pia ina habari ambazo mara nyingi hazipatikani kwenye vyombo vya habari vya kigeni kuhusu Japani, kama mwanaume ndani ya vazi la Godzilla .

Utafiti wa Utamaduni wa Japani

Ikiendeshwa na Jake Adelstein, mwandishi wa habari za kiuchunguzi amnayeandika habari za uhalifu jijini Tokyo inayashinda magazeti ya kila siku yanayoandikwa na Kijapani, Utafiti wa Utamaduni wa Japani ni mahali unapoweza kwenda kupata habari za udaku wa hivi karibuni na habari za kiuhalifu, uovu, siasa za kifisadi na “upande wa giza wa Jua Linalochomoza.”

Kitabu cha Adelstein Tokyo Vice[Uovu wa Tokyo] inafaa kusomwa, huku kukiwa na tetesi kwamba hivi karibuni itakfanywa kuwa sinema.

Tofugu

Nyota inayochomoza kwenye ulimwengu wa blogu za Kiingereza nchini Japani, Tofugu huandika ubunifu mzuri na maoni yanayovutia kuhusu utamaduni maarufu wa Kijapani.

Simulizi moja wapo la kuvutia la habari zinazoandikwa na blogu ya Tofugu hivi karibuni ni mahojiano ya pili kwenye YouTube na mitandao ya kijamii yaliyofanywa na Medama-sensei.

Sasa akisoma kwenye shule ya dini ya Zen, Medama-sensei aliwasha mjadala mkali aliposifia na kulaani kutangazwa kwake kwenye mtandao wa YouTube kwa unyanyapaa wakati wa ziara yake kama mwalimu wa shule wa Kiingereza huko Okinawa. 

Una suala la ziada kwenye orodha hiyo? Tufahamishe kwenye maoni!

1 maoni

  • Mashauri Joseph

    Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri mnazoendelea kufanya za utoaji wa habari mbalimbali ili kuweza kuwafahamisha wengina yanayojiri katika mataifa mengine yaliyoendelea. Nawaapa moyo katiksa hili muendeleee kusonga mbele zaidi na zaidi….

    Mashauri Joseph toka Mwanza Tanzania

Sitisha majibu

jiunge na Mazungumzo -> Mashauri Joseph

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.