Hali ya Kusikitisha Katika Kituo cha Magarimoshi cha Mumbai

Mwanablogu Antarik Anwesan anaelezea hali halisi ya kile kinachoendelea katika kituo cha magarimoshi cha Goregaon kilichopo Mumbai, India. Gari moshi lifanyalo safari za ndani liliondoka kituoni bila ya kutoa taarifa wakati abiria walipokuwa wakiharakisha kuingia. Kadri ya garimoshi lilivyoongeza mwendo, watu wawili walianguka kupitia mlangoni, chupuchupu kupoteza maisha. Taarifa ya tukio hili haikuripotiwa katika kituo chochote cha habari. Mwanablogu huyu afafanua kuwa, pamoja na kuwa waathirika katika magarimoshi yafanyayo safari za ndani huongezeka kila mwaka, serikali haijaweza kuweka mikakati ya usalama wa usafiri wa magarimoshi unaotumiwa na watu wengi zaidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.